SERIKALI YATAKIWA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI KATIKA UPANGAJI WA MIPANGO.



  Na Stephen Noel -Mpwapwa.
SERIKALI imeobwa kushirikisha sekta binafsi katika upangaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo ili kuweza kuwa na nguvu moja  katika kuzikabili changamoto za kimaendeleo zinazotokana na serikali kuto  shirikisha sekta hiyo.
Lai hiyo imetolewa na  Bwana  Dornard Liya  mshuari wa  mradi wa  kuboresha  mazingira ya uwekezaji  na biashara  Tanzania unaotekelezwa na shirika la  Denmark  katika mikoa ya Dodoma na Singida alipokuwa akiongea na wafanya biashara  wilayani mpwapwa mkoani Dodoma.
Dornard alisema  kutokana na utafiti uliofanywa na shirika  hilo ulibaini kuwa  katika  nchi ya Tanzania  kumekuwa na mazingira   magumu ya ufanyaji wa biashara  kwa wafanya biashara unao tokana na kulundikiwa kodi kandamizi kwa wafanya biashara hao  na kutoshirikishwa katika  upangaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwa  sekta binafsi.
Aliongeza kuwa   historia ya  ya nchi yetu ya ujamaa na kujitegemmea pia imeadhiri kutozipa kipaumbele sekta binasfi katika upangaji wa mipango ya serikali kitu alicho kisema kuwa kinapelekea kuwepo  malalamiko mengi  kutoka kwa sekta hiyo kwa serikali.
Pia aliongeza kuwa kuwepo kwa baadhi ya sheria ndogo za  kodi za halmashauri zimekuwa  kandamizi na kupelekea  wawekezaji wengi   kuyakimbia mazingira ya kuwekeza katika halmashauri nyingi hapa nchini kutokana na urasimu kwa baadhi ya watendaji wa tasisi hizo
Hata hivyo alisema tafiti zinaonyesha  kuwa Tanzania imekuwa inashika kuanzia nafasi 145 kati ya nchi 189  duniani  kitu alichokisema  kuwa  kinasababishwa na urasimu wa Sera, sheria  na kanuni  za biashara nchini.
Hivyo  aliwataka wafanya bishara  wilayani hapo kuweza  kuunda  baraza la  biashra la  wilaya ili kuweza kufanya ushawishi  na utetezi  juu ya sera, na sheria  kandamizi za kikodi.
Kwa upande wake mwenyekiti  TCCIA wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  bwan Ben Mosha alisema  wafanya biashara kuto kuwa na umoja  umekuwa ni kikwazo cha wafanya bishara hao kukosa sauti ya pamoja  juu ya kufanya ushawishi na utetezi  kwa sheria zinazotishia  uendelevu wa  bishara unaotokana na  mlundikano wa Kodi.
.
Mmoja wawafanya biashara  mdogo wilyani hap Judith Tomas alidai kuwa  Kikwazo  kikubwa cha  wafanya biashara wilayani hapo kushidwa  kukua kiuchumi  ni kukosekana kwa miundo mbinu ya kuaminika hasa barabara  za kuiunganisha wilaya  hiyo na barabara kuu ambayo walisema ingeweza kuwa kichocheo kikubwa cha wawekezaji  kuwekeza katika wilaya hiyo.
Alisema kitu hicho  ndicho kinachoifanya  wilaya hiyo kuonekana kama  iko ndani ya kisiwa na kuanza kuzidiwa kimaendeleo na wilaya  amabazo  zimezaliwa kutoka katika wilaya  hiyo kama wilaya  ya Kongwa.
Magnus Msafiri  alisema  kuwa pamoja na wafanya biashra  wa wilaya hiyo kukwazwa na kuto kuwepo kwa elimu ya kikodi kwa wafanya biashara  hao  pia kumekuwako na mahusiano hasi kati  wafanya biashara  hao na watumishi wa halmashauri hiyo .
Alisema  japo kuwa  Mpwapwa ina fulsa za kutosha juu ya uwekezaji lakini  viongozi wa wilaya hiyo kuto fungua milango ya uwekezaji na kuitnagza wilaya hiyo  pamoja  na fulsa zinazo patikana  ndani ya wilaya hiyo imekuwa ni sababu ya wilaya hiyo kusua sua kimaendeleo.
 Pamoja  na  kikao hicho viongozi hao  waliweza kuteuwa uongozi utakao weza kuunda baraza la bishara la wilaya ambao ni ,Ben mosha, Efrahim George,Monica Lumambo,Joseph Mnemele, na Efrasia  Mrema.

Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.