WANAFUNZI WA AWALI IDILO MPWAPWA WASOMEA CHINI YA MITI.




WANAFUNZI WA awali katika shule  ya msingi  Idilo  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  huwalazimu kusomea chini  ya miti kutokana na  uhaba wa vumba vya madarasa sheleni hapo.
Wanafunzi hao waliokutwa  na majira  wakiwa wamekaa  kwenye viti  vya matofali huku wakiwa chini miti na darasa linaendelea.
Ofisa elimu kata ya Mazae Bwana Betweli Sanga   alikili wanafunzi hao kusomea chini ya miti kitu alicho sema kinasababishwa  na uhaba wa  wa vyumba vya madarasa  katika shule hiyo.
Sanga  alisema kwa  sasa shule hiyo inavyumba vya madarasa  7 wakati mahitaji ni  vyumba 10 na kupelekea kuwa  upungufu wa vyumba  vitatu  vya madarasa  shuleni hapo.
Sanga alisema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 290 wakiwamo wavulana 129 na wasichana 120lakini inavyumba saba vya madarasa.
Aidha Sanga alisema pamoja na uhaba wa vumba vya walimu pia shule hiyo inakabiliwa na chanagamoto ya nyumba za walimu,matundu ya vyoo,pamoja na vifaa vya kufundishia
Kufuatia hali hiyo uongozi wa kijiji hicho  umeamua kijenga chumba  kimoja cha wanafunzi hao  ii kuweza kuwandoa wanafunzi hao kusomea kwenye miti kukaa chini  na kuwataka  wasomee kwenye darasa la kisasa lenye hadhi ya kusomea  wanafunzi wa awali ambalo litakuwa na ofisi yake pamoja  choo chake  ili kuyaboresha mazingira  ya watoto hao kupenda shule.
Kwa mujibu  wa  mwenyekiti  kijiji cha Idilo bwana  Grasion Mkokoten alisema wameamua kufanya  hivyo  kutokana ni wajibu wao kama serikali ya kijiji pamoja na wananchi wa kijiji hicho kuweza  kushiriki katika maendeleo yoyote katika kijiji chao  ili serikali iweze kuwaunga mkono katika umaliziaji.
Bwana mkokoteni alisema kutokana na  wanafunzi hao kusomea chini ya miti kumepelekea wanafunzi wengi wa awali kutopenda shule ,hivyo kusababisha wazazi wengi  kuto kuandikisha wanafunzi hao walio fikia umri wa kuanza darasa la awali kuto andikishwa.
Hata hivyo Mkokoteni alisema wao kama kijiji watajenga darasa hilo hadi kufikia kiwango cha boma  na pia watashiri kisha wadau wa Elimu kote nchini pamoja na nguvu ya serikali kwa ajili ya umaliziaji

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.