DC atangaza vita na waharibifu wa mazingira mpwapwa.


 Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri ametangaza vita na watumishi wa serikali watakao bainika katika  kuihijumu serikali  katika vita ya kupambana  na uharibifu wa mazingira Mpwapwa.
Shekimweri aliyasema hayo ofisi kwake alipo kuwa akiongea na  waandishi   juu  mikakati ya kuikomboa wilaya hiyo juu ya uharibifu  wamazingira.
Mkuu wa wilaya hiyo alisema    kupitia kamati ya ulinzi na usalama imebaini baadhi ya watumishi wa serikali wamekwa wakihusika katika uharibifu wa mazingira kwa  kuwa na vibali feki ya kuchana mbao .
Aidha alisema  watumishi wote waliotuhumiwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakama  kujibu tuhuma zinazo wakabili.
“Inasikitisha kuona watumishi wenzangu wa serikali  kujikita  katika sula la uharibifu wa mazingira ,kwa hili sitakuwa na uvumilivu hata kidogo katika mazingira mimi nina zero tolelance lazima wote wachukuliwe hatua na wafikishe mahakamani.”aliongea  
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  Jabir Shakimweri alisema kuwa tadhimini iliyo fanywa na  Baraza la mazingira Tanzania NEMC  limebaini kuna  baadhi ya madahara yanayo tishia  uendelevu wa wilaya hiyo kiuchumi na kijamii.
Shekimweri alisema kwa sasa  kuna uharibufu mkubwa wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mpwapwa  kitu alicho sema kuwa kinatokana   na baadhi ya ya viongozi kushidwa kusimamimia  sheria ,uzembe ,kuzoeana na mianya ya rushwa kuanzia kamati za mazingira  ngazi za vijiji  na kata.
Aidha Shekimweri  kufuatia hali na  hiyo imeonyesha kuwa Mpwapwa siku si nyingi inaweza kugeuka jagwa kutokana na wananchi kulima  katika vyanzo vya maji, kuchoma mazingira,na kulima katika misitu ya uhifadhi pamoja na kukata miti ya asili iliyo kuwa chanzo kikuu cha kuvuta maji katika ardhi.
 Pia alisema kufutatia  taarifa hiyo   kumenyanyua kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya    kuweza  kuweka mikakati  kabambe ya kuirudisha Mpwapwa katika uoto wake wa asili kama ilivyo kuwa asili kwa kuweka uhamasishaji,kuweka mikakati ya usimamizi wa sheria  kwa kujengea uwezo mabaraza la kata pamoja na kamati za mazingira ngazi za vijiji hadi kata.
“Kwa kweli mimi kama mkuu wa wilaya sitakiwi kulalamika  ninachotakiwa kukifanya ni kutoa majibu katika hiki kisicho kuwa na  majibu  hasa katika mazingira ,kwa kweli sina uvumilifu hata kidogo tumeweka mikakati kababmbe ya kuirudisha mpwapwa katika uoto wake wa asili  kama ilikuwa awali”aliongea Shekimweri.
Alisema  matokeo ya uharibifu wa mazingira ni mkubwa  ambapo katika vyanzo vya maji vya mtililiko katika mji wa Mpwapwa  vilivyo kuwapo ni chanzo kimoja tu ambacho kimebaki cha Mayawile nacho kikendelea kukauka kila kukicha .
Alisema kuwa  Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambazo haziko vizuri katika utanzaji wa mazingira na misitu ya asili kwa watu kuchoma ,kulima  na kukata miti katika vyanzo vya maji na katika vilele vya milima .
 Aliongeza  kuwa tayari wilaya ya Mpwapwa  imeshanza kukubwa na matokea ya tabia ya nchi kwa kuongezeka kwa joto, kupungua kwa mvua na kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji ambayo vilikuwa ni tegemeo kubwa kwa maisha ya wakazi wa mpwapwa na viunga vyake kwa kuendesha maisha ya kila siku.




Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.