AFUGWA JELA KWA PASI YA MKAA YA SHILINGI 2000.




Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya  ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma   imemuhukumu kifungo cha mwaka 1  jela  mwalimu wa  shule ya msingi Mtamba  kata ya rudi  wilaya ya Mpwapwa kwa kosa la pasi ya uwizi ya shilingi 2000/=
Kesi hiyo iliyokuwa kesi ya rufaa kutoka katika mahakama ya Mwanzo Chipogolo na  ikisikilizwa na hakimu mkazi   wa mahakama   ya wilaya   bwana Paskal Mayumba.
Mtuhumiwa huyo   ambae alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Mtamba  alidaiwa kutuhumiwa kwa kosa la kuvunja na kuiba  mali kadhaa za Bi  Zena Hoseaikiwa ni radio moja ,pasi ya mkaa na na una kilo kumi.
Hakimu Mayumba  alisema kuwa  mtuhumiwa huyo  alifanya kosa hilo  kinyume na  kifungu cha sheria namba 273 C ya kanuni ya adhabu  sura  namba16
“Kwa  mujibu wa kifungu hicho  sheria ambacho kinatamka wazi kuwa kama mtu aliyepatikana na hati na kuvunja na kuiba  ni mika 14 jela kwa kosa la kuvunja na miaka7”aliieleza mahakama hakimu Mayumba.
Akipewa nafasi ya kujitete mtuhumiwa hayo  aliomba mahakama ipunguzie adhabu kwa kuwa ana majukumu ya serikali pia na familia yake ikiwemo wazazi wake  na watoto wa ndugu zake ambao anawasomesha  na wanamtegemea pia  ni kosa lake la kwanza. 
Hakimu Mayumba alisema   kutokana na   mwenendo wa kesi    “hivyo mahakama inakufunga mwaka 1 jela .”aliongea hakimu Mayumba.
Na alisema kwa mtu yeyote ambae hajaridhika na adhabu hiyo ana haki ya kukata  rufaa ndani ya siku thelathini.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.