DC agundua chang za maji mpwapwa.

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akikagua baadhi ya mitambo ya maji katika kisima cha Kiombo.




ZAIDI ya wakazi  29,422 wa mji wa mpwapwa na viunga vyake hutumia maji machafu  yasiyo tishia kutokea kwa magonjwa ya mlipuko  yanayosababishwa na matumizi maji maji machafu.
Hali hiyo imebainishwa na Mkuu wa wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri  baada ya kutembelea vyanzo vya maji vinavyo saidia  kusambaza  maji katika mji wa  Mpwapwa.
Pia Shekimweri abaini  changamoto lukuki zinazosababisha Mji wa Mpwapwa kuto kuwa na maji ya uhakika japo ya kuwa na mradi  mkubwa wa maji ulioghalimu jumla ya shilingi billion4.
Aidha changamoto zilibainishwa na mkuu wa wilaya hiyo ni maji yanayotumiwa na wakazi mpwapwa ni machafua ambapo tumbili,Ngedele na wanyama wa poli kuyatumia na kuoga  humo kutoka na chanzo hicho kutokuwa  na uzio  wa kuweza kuzuia wanyama kuchafua kwenye vyanzo hivyo.
Pia ufanisi hafifu wa mradi  wa maji chumvi ujulikanao kama mradi wa mkenya iliogharimu jumla ya shilingi billion 4/= uliofadhiliwana serikali ya Kifaransa uliojegwa na kampuni ya Oliento kutoka nchini Kenya ambao ulitegemewa kuwa mkombozi wa adha ya maji katika mji wa Mpwapwa, ambapo hali hiyo imekuwa tofauti  kwa mradi huo ambao kwa sasa wakazi wa mji wa mpwapwa hupata maji kwa zamu kwa siku moja hadi mbili kitu kinachowatia wasiwasi  wakazi wa mpwapwa kuwa labda mradi huo na vifaa vilivyo wekwa haviendani na thamani  ya fedha.
Kufuatia hali hiyo  mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  ametoa  siku 30 kwa mamlaka ya maji mjini hapa MPWAUSA  kuweza kufanya malekesho yote kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kuyafanyia usafi matanki yote  yanayosaidia kusambaza maji katika mji wa mpwapwa,  ili kuweza kujikinga na magonjwa ya mlipuko na magonjwa mengine yanayo sababishwa na kutumia maji machafu.
Kwa  upande wake  mkurugenzi wa  mamlaka wa maji safi na Mazingira MPWAUSA  Bwana Peter Kabelwa  amekili mradi huo kutoa huduma chini ya kiwango, ambapo alisema kwa maelekezo ya mradi yalitakiwa mashine zizalishe  maji ujazo wa lita 80,000kwa saa lakini kwa sasa mashine hizo huzalisha lita 45,000 kwa sasa tofauti na maelekezo ya mradi.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa mamlaka ya   tumejipanga kufanya uchunguzi wa uwezo wa mashine zilizo wekwa kwa ajili ya usambazaji wa maji mjini hapa kitaalamu tunaita (Pumpu tsting)aliongea

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.