WALIMU WAUNGA MKONO MGOMO KWA ALMIA 98.4 MPWAPWA

Na  noel Stephen mpwapwa
30 julai 2012
 Asilimia 98.4 ya walimu wote wa wilaya ya mpwapwa waunga mkono mgomo wa walimu unaoendelea kote nchini  wakati asilimia 1.6 hawakubaliani na mgomo huo.

 Ni kauli  iliyo tolewa na mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani  mpwapwa  Bi NELEA NYANGUYE mkoani dodoma  alipokuwaakiongea na waandishi wa habari  ofisi kwake juu ya kutoa msimo  wa chama hicho juu  mgomo wa walimu wote katika wilaya ya mpwapwa.

Bi nyanguye  alisema kufuatia  kauli ilioyo tolewa na  Raisi wa chama hicho taifa  wilaya ya mpwapwa imeunga mkono kwa asilimia  98.4 mgomo huo  kwa kuishinikiza serikali kuwalipa haki zao za msingi kama watumishi wa serikali .

Aidha bi Nyanguye alisema kuwa  kufuatia  kifungu cha 80 kipengele kidogo cha (1)d  cha sheria ya mahusiano kazini  ya mwaka  2004  walimu ambao ni wanachama wa CWT walianza zoezi la kupiga kura  tarehe 25 julai 2012 na  kumalizika tarehe 27julai na na asilimia 98.4 ya walimu wote wa wilaya ya mpwapwa waliunga mkono  mgomo huo.

 Alisema   wilaya ya mpwapwa  ina walimu 1491  ambao waliunga mkono ni walimu  1470 ambapo alisema kuwa walimu 21 hawakuunga mkono mgomo huo.

 Na alidakuwa mgomo huo unahusuisha walimu wa shule za msingi,  sewkondari,  vyuo vya ualimu ,na chuo cha maendeleo ya  jamii  (FDC)

Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya  hiyo bwana Musa  Singo siku siku ya  ya mgomo alikuwa akitembelea  mashuleni akiwa ameambatana na afisa elimu taaluma  sekondari na Afisa Elimu taluma msingi wakiwa wakiwataka wallimu walio fika shuleni hapo  na kupiga sogo ofisini kuwataka waingie madarasani na kufundusha huku akiwajazisha fomu ya mgomo  kwa walimu walio kuuwepo katika shule hizo .

 Bwana  Singo akitakiwa kuelezea  mgomo huo kwa waandishi wa habari aligoma kulisema hili na kuwataka waandishi wa hanbari kwenda kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule  msingi chgazungwa  ambapo ndipo alipokutwa na wandishi wa habari akiwashawishi walimu kuachana na mgomo huo .

Kwa upande wa  afisa elimu huyo na kuingia madarasani  na  kuanza kufundiisha japo kwa kwa shingo uypande  lakini wengine waliendelea na msimamao wao wa kukaa ofisini na kuendelea kupiga sogo

 K atika  shule nyingi hapa mpwapwa zilionekana kuto kuwa na walimu wakati walimu wengi wakiwa wamesaini katika kaitabu cha mahudhurio ya kila siku lakini hawakuwepo madarasni .

Na pia imeadhili zoezi zima la wanafunzi ambao walitakiwa  kuanza mitihani ya kufungia  shule lakini wanafunzi wengi walionekana wakilandalanda kwenye viunga vya shule hizo bila kujua muelekeo wao..


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.