KIKOSI CHA USALAM CHA WANAWAKE CAANZISHA UPYA

Kambi ya kikosi cha polisi cha huduma za haraka ambacho kinafanya kazi pamoja na jeshi kupambana na ugaidi na kutoa usalama wa hali ya juu kwa maofisa nchini Somalia kilifunguliwa tena katika wilaya ya Wardhigley huko Mogadishu wiki iliyopita.
  • Ofisa wa polisi wa serikali ya Somalia akiweka ulinzi wakati msafara wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ukipita Mogadishu mwezi  tarehe 23, Februari 2012. [Na Mustafa Abdi/ AFP) Ofisa wa polisi wa serikali ya Somalia akiweka ulinzi wakati msafara wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ukipita Mogadishu mwezi tarehe 23, Februari 2012. [Na Mustafa Abdi/ AFP)
Kitengo cha The Darawish asili yake kilianzishwa na Jenerali Mohamed Siad Barre miaka ya 70 kama kikosi cha taifa cha jeshi la polisi; kikaacha kufanya shughuli zake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kutokana na mizozo ya miongo miwili iliyopita.
Ujenzi upya na ukarabati wa kituo cha zamani huko jirani na Agadhiig ulikamilika hivi karibuni, na kilifunguliwa tena rasmi tarehe 26 Julai
Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, waziri wa nchi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdi Ahmed Ali, Kamishna wa Kikosi cha polisi cha Somalia Sharif Sheikhuna Maye, pamoja na makamanda wa polisi, bendi ya muziki ya taifa na wanachama wa Darawish walihudhuria sherehe za ufunguzi.
Akiongea na wanachama wa Dawrish, rais huyo alisema, "Kazi yenu ni kutoa usalama, kulinda maofisa na kupambana na ugaidi. Mnatakiwa kufanya jukumu kubwa katika maeneo haya yaliyokombolewa kutoka kwa al-Shabaab na kutoa huduma kwa wakazi wa ndani."
"Polisi wanapaswa kudhibiti kitengo hiki kwani wanawajibika na uangalizi wa maelekezo ya usalama na kuhakikisha yanatekelezwa kutokana na sheria na kanuni," alisema Ahmed.
Ali alisema wizara yake iliandaliwa kuongeza kiwango cha Darawish kupitia mafunzo kutoka katika nchi zinazoendelea. Alisema kufunguliwa upya kwa ngome ya Darawish kutakuwa na dhima muhimu katika mafanikio ya oparesheni za pamoja kati ya polisi na huduma za kipelelezi.
Mwana mikakati ya usalama Farhia Faarah Iidle alisema wanachama wa zamani wa al-Shabaab walijitoa katika kundi na kujiunga na kundi la Darawish ili kusaidia kazi za upelelezi za kuwasaka masalia ya kundi linalojihusisha na al-Qaeda na wapiganaji wageni nchini Somalia.
Iidle alisema Darawish wapo katika mchakato wa kuwalenga magaidi waliojificha na vituo vyao vya ugavi wakiwa na lengo la kushurutisha upotevu mkubwa dhidi ya vyeo vya al-Shabaab waliobaki Somalia ya kati na Kusini.
Jeshi jipya la Darawish linahusisha pia wajumbe wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu ambao walirudisha vyeo na kuingia katika polisi baada ya kukamilisha kozi ya mafunzo nchini Kenya, Uganda, Jibuti na Uturuki, maelezo hayo yalitolewa na mchambuzi wa masuala ya siasa Mohamed Aadan anayeishi Mogadishu.
Aadan aliiambia Sabahi kwamba serikali ya mpito ilipewa sifa njema ya kijamii kwa wajumbe wa Mahakama ya Kiislamu, pamoja na mafunzo ya kijeshi yaliyokusudiwa kuwahusisha katika kitengo cha Darawish cha jeshi la polisi. Alisema wanamgambo wa zamani walipewa mafunzo kuhusu maarifa ya washirika wa al-Shabaab na wanaowaunga mkono.
"Jeshi jipya la Darawish limepewa taarifa ya kutosha kuliko majeshi mengine linapokuja suala la kutambua nyuso na kufichua ukweli kuhusu wapiganaji wa al-Shabaab," alisema.
Kamishna wa Polisi Maye alisema kwamba kufunguliwa upya kwa ngome baada ya miaka 21 ni chanzo cha furaha kubwa kwa washirika wa kitengo cha Darawish, ambao awali walikuwa wakipanga katika majengo yaliyobomoka.
Alisema operesheni za Darawish zitashirikishwa katika mafanikio ya maendeleo ya kundi na kumaliza vurugu na ugaidi uliohamasishwa na al-Qaeda waliohusishwa na kundi la al-Shabaab.
"Miaka mitano iliyopita nilikuwa mwanamgambo wa kundi la wanamgamboo wa Mahakama ya Kiislamu, lakini kwa hiari yangu nilijiunga na jeshi la polisi la nchi mwezi Aprili, 2009 hadi kuanzishwa upya kwa Darawish kulipotangazwa," Abdiqadir Haji Hassan, mwanajeshi wa kikosi cha polisi cha Darawish, aliiambia Sabahi. Alikubali kwamba washirika wa zamani wa jeshi la Darawish wamerejeshwa upya na mataifa yaliyoungana.
"Mimi ni kituo cha ukaguzi huko Mogadishu, Udhibiti X wa Afgoye, ambao unakagua magari yote, magari ya mizigo na hata watu wanaojaribu k

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.