BUNGE LA SOMALIA LAPANAGA

Bunge la Taifa la Katiba ya Somalia (NCA) lilifungua siku yake ya sita hapo Jumatatu (tarehe 30 Julai) ambapo wajumbe waliahidi kutochelewesha zaidi wakati wanafanya kazi kuelekea uidhinishaji wa rasimu ya katiba ifikapo tarehe 2 Agosti, kwa mujibu wa Redio Mogadishu.
  • Wajumbe wakihudhuria sherehe za ufunguzi wa mkutano wa Bunge la Taifa la Katiba tarehe 25 Julai. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi] Wajumbe wakihudhuria sherehe za ufunguzi wa mkutano wa Bunge la Taifa la Katiba tarehe 25 Julai. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi]
Wajumbe 825 walikutana tarehe 25 Julai katika Chuo cha Polisi Mogadishu na kuanzia hapo kukutana kila siku isipokuwa ucheleweshaji wa muda siku ya Ijumaa kutokana na sababu za kiufundi na shambulio la kombora karibu na hapo. Hakuna aliyejeruhiwa katika mlipuko huo.
"Licha ya vikwazo vilivyopo na ucheleweshaji uliokuwa unajirudia rudia, kufunguliwa kwa mkutano wa NCA ni hatua muhimu katika historia ya Somalia," Abdiqadir Yusuf, mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliyeko Mogadishu, aliiambia Sabahi.
"Baada ya miaka 21 ya vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe, bila ya kutaja ugaidi na uharamia, Wasomali wanaweza kuamua hatima yao wenyewe ndani ya nchi yao kupitia mchakato wa kidemokrasia," alisema.
"Hii ni hatua ya kihistoria na wakati wa kuwa na hisia chanya kwa Wasomali wote," alisema. Somalia inakaribia mwanzo mpya na kuunda taifa ambalo linaweza kurejesha amani na utulivu nchini."
Wakati rasimu ya katiba imechochea majadiliano miongoni mwa Wasomali, huku wengine wakiita sio ya Kiislamu au ni ya kisekula sana, wengi wameelezea hisia zao kwa mchakato huu ambao utamaliza kipindi cha serikali ya mpito.
Hapo Alhamis, mamia ya wakazi wa Mogadishu waliingia mitaani kuelezea kuwaunga mkono kwao wajumbe wa NCA. Waandamanaji waliwataka wajumbe kuidhinisha katiba mpya, wakibeba mabango yanayosomeka, "Watu wanataka mageuzi ya kisiasa" na "Katiba mpya inawa

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.