WANAKIJIJI WAMKATAA MWEKEZAJI WA MADINI LUFUSI

NA noel Stephen mpwapwa.
MKUU  wa  wilaya ya Mpwapwa Bwana  CHRISTOPHER KANGOYE  amesitisha  uchimbaji wa madini aina ya copa   katika kata ya lumuma kijiji cha LUFUSI  kwa kampuni ya  KIMANI MINERALS LIMETED kufuatia kuto fuata taratibu na uharibifu wa  mazingira .

MKUU huyo amefikia hatua hiyo kufuatia mgogoro ulioibuka kati ya mwekezaji huyo na  wanakijiji  wa kijiji hicho kwa madai kuwa  mwekezaji huyo hajafuata  taratibu za uchimbaji wa madini na  kuchimba madini hayo karibu na vyanzo vya maji vya kata nzima ya lumuma  na  vijijiji vyake.

AKIONGEA na waandishi wa habari   ofisini  kwake  bwana KANGOYE  alikili kuwepo kwa mgogoro kati ya mwekezaji wa huyo na wanakijiji wa kijiji cha lufusi  kwa madai kuwa  amechimba madini hayo karibu na chanzo cha maji cha kijiji hicho na  ambacho ni tegemeo la upatikaji wa maji  wa kata ya lumuma na vitongoji vyake.

AIDHA KUU huyo alisema kuwa  kampuni yenye leseni ya wachimabaji wadogo lakini wanatumaia  mitamabo ya kisasa katika kufanya utafiti wao maboa kwao umejikita katika kuitafuta faida na kuwadhoofisha wazawa na mali zao  za asili” nasema lazima tuangalie faida ya wengi na sio kuangalia  faida za wachache  kwa sababu siku hizi  watu hao wanataka faida yao tu  na si watu wengi na lazima tutunze mazingira  ili yaweze kutusaidia badae.

Pia  B wana Kangoye aliwa taka watu wote wanao ishi kwenye vyanzo ya maji vya kijji hicho  lazima waondoke wenyewe kabala hajatumia  nguvu za dola kwa ajili ya msatakabali wa wilaya ya mpwapwa na vitongoji vyake “ nasema hakuna aliye juu ya sheria  hivyo wito wangu kwa wananchi na wawekezaji wafute sheria na taratibu ili kuiendeleza mpwapwa”

Alivitaja vijiji  ambavyo  wakazi wake wanaendesha shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji alisema kuwa ni kijiji cha Lufusi kata  ya lumuma, kiboriani mpwapwa mjini na kwamdyanga kata ya mpwapwa mjini nakuwataka wahame maeneo hayo kabla hajatumia nguvu za dora.

KWA UPANDE wake meneja wa maradi wa  shirika la kuhifadhi misitu ya Asili ya  Tanzania  Bwana  LAURENT MWAKAKONYOLE  alidai kuwa wawekezaji hao wameingia kwenye msitu wa asili ya kata ya lumuma na kuharibu misitu na wamechimba barabara yenye urefu wa km 8 katikati ya msitu bila kuhusisha uongozi wa kijiji   amabapo alisema ni ukiukaji kwa kanuni na taratibu za nchi.

Mwakakonyole  alisema shirika lao limejikita  katika kuhifadhi misitu ya asili  ya  safu za milima ya Lubeho ambako zimeonyesha  mafanikio makubwa ya kumbamabana na  mabadiliko ya hali ya hewa nchini na kutunza  uoto wa asili  katika milima  ya LUFUSI kata ya lumuma .

Mtendaji wa kata  kijiji hicho  BWANA  Jonas MBOGO  aliwataka wananchi  wa kijiji hicho kufuata sheria na taratibu  ili kuweza kutunza mali asili zao kwa kushirikiana na wadau  wanaojitokeza katika kijiji chao kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

ALISEMA kijiji chake kimejikuta kimeingia  kwenye mgogoro na mchimbaji wa madini hayo kwa kukiuka  sheria ya madini ya mwaka 2010 namba  95kifungu kidogo cha (1)(a) na (iv)kifungu kidogo cha pili (II) na cha (V)(c)na (e).

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.