JKT VIGOGO KIZIMBANI


*Wadaiwa kuhamisha Sh bilioni 3.8 kinyemela

MAOFISA saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao ni wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya SUMA JKT, wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia madaraka vibaya na kuhamisha Sh bilioni 3.8 kutoka akaunti ya Bodi ya Zabuni ya Ushirikiano wa Tanzania na Korea (TAKOPA), kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao, walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana na kusomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Beny Linkolin.

Linkolin, aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Kanali Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali, Mkohi Kichogo, Luteni Kanali, Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajenti John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali, Felix Samillan.

Alidai washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka saba, shtaka la kwanza linawahusu wote, ambapo inadaiwa Machi 5, 2009 katika ukumbi wa mikutano uliopo SUMA JKT mjini Dar es Salaam, wakiwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji na Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya SUMA JKT, walitumia vibaya madaraka yao.

Alidai washitakiwa waliruhusu Bodi ya Zabuni ya SUMA JKT, kufanya kama Bodi ya Zabuni ya TAKOPA, kwa lengo la kununua magari chakavu na vifaa vya ujenzi bila kupata kibali kutoka Bodi ya Wakurugenzi ya TAKOPA.

Shtaka la pili, linawakabili washitakiwa wote, ambapo inadaiwa Machi 12, 2012 mjini Dar es Salaam, walinunua magari chakavu na vifaa vya ujenzi kinyume na sheria ya ununuzi.

Mwendesha mashitaka huyo, alidai shtaka la tatu linamkabili mshitakiwa wa pili, Luteni Kanali Samillan na wa tatu, Luteni Kanali Kichogo ambao wanadaiwa Machi 16, 2009 mjini Dar es Salaam, walihamisha Sh 2,744,432,545 kwa kutumia hundi namba 000010 kutoka akaunti ya TAKOPA, namba 011103031753 kwenda katika akaunti ya SUMA JKT, namba 0111030794 zote ziko benki ya NBC kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao, pia wanakabiliwa na shtaka la nne, wanadaiwa kinyume cha sheria Aprili 3,2009 walihamisha Sh 489,677,878.30 kwa hundi namba 000011 kutoka akaunti ya TAKOPA namba 011103031763, kwenda katika akaunti ya SUMA JKT, namba 011103017094 zilizopo benki ya NBC.

Shtaka la tano, linawakabili washitakiwa hao ambapo inadaiwa Aprili 4, 2009 Dar es Salaam, walihamisha Sh 269,519,093.60 kwa hundi namba 000012 kutoka akaunti ya TAKOPA namba 011103031753 kwenda akaunti ya SUMA JKT namba 011103017094 kinyume na sheria.

Pia washitakiwa hao, wanatuhumiwa katika shtaka la sita, inadaiwa Aprili 4, 2009 wakiwa Dar es Salaam kwa kutumia hundi namba 000015, walihamisha Sh milioni 350 kutoka katika akaunti ya TAKOPA namba 000003031753 kwenda SUMA JKT akaunti namba 011103017094 zote za NBC.

Linkolin, alidai shtaka la saba linawakabili washitakiwa wote, wanadaiwa kati ya Machi na Mei, 2009, walikula njama na kuhamisha fedha kutoka akaunti ya TAKOPA namba 011103017094 iliyopo benki ya NBC kinyume cha sheria.

Washitakiwa wote walikana mashitaka na m

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.