WAZAZI WASHAURIWA KUWAKEZEA WATOTO.



 Wito  umetolewa kwa wazazi wote nchini kujenga moyo  wa kuwawekekea watoto wao akiba  mbali mbali za kimaisha  ili wasipate taabu  wanapo ingia utu uzima

 Wito huo umetolewa na Meneja wa Bank  ya  NMB  tawi la Mpwapwa BWANA HERMAN MASUKI  hivi karibuni alipo kuwa akizindua   mpango wa    Ankaunt maalum kwa watoto  walio chini ya miaka kumi na nane ajulikayo kama  Finacial Fitness .

Bwana masuki alidai kuwa Wazazi wengi nchini hawana  tabia ya kuwawekea akiba watoto walio chini ya miaka kumi na nane  kitu alicho kisema kuwa kina leta shida pindi mtoto aingiapo utu uzima na kuanza au anapo pelekwa shule kushidwa kugalamiwa masomo kutokana na wazazi wengi kuto kuwa na malengo ya badae kwa watoto wao



Mhasibu wa  BENK  ya NMB Mpwapwa akitoa zawadi kwa wanafunzi  walio hudhuria harmbee  ya fitness  M pwapwa (picha na noel Stephen mpwapwa.



 Bwana  Musuki  alidai kuwa  wazazi waweze kuwa fungula watoto wao akaunti ijulikanyo kama junior account  amabayo alisema kuwa  ni ankunti iliyo wekwa mahususi  kufundisha watoto njisi ya kuweka fedha  kwa ajili ya matumizi ya baadae.


Alisema  kuwa wazazi wakumbuke kuwa  “iku zote  maandalizi ya kesho yaanaanza leo kwahiyo naombeni wazazi nanyi watoto kuweza kujenga tabia za  kujiwekea akiba  ili kuweza kuondoka na hali ya kujuta baadae”.

Aidha alisema kuwa watoto wengi wamejikuta wanaingia kwenye shida  au matatizo  kutokana   kuto kuwa na akiba ya kuanzia maisha au kjiendeleza kibiashara  na masomo.

 Pia “tukumbukle kuwa sisi hatuna mkataba na mungu  je watoto wangapi ambao tunawaona wazazi wao walikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha lakini mala baada ya kufa  wazazi wao tunawaona watoto wanapolwa mali na ndugu wa marehemu na kubaki hawana kitu na kuwa watoto wa mitaani je wangewekewa akiba benki nani angewadhurumu hivyo ndugu zangu tupende  kujijengea tabia  ya kuwawekea watoto  akiba za maisha”aliongea bwana Masuki

ALISEMA kuwa Benki  hiyo imeamua kuanzisha  mpango huo kufuatia tafiti mbalibali zilizo fanywa na  maafisa ya benki hiyo na kugundua kuwa watoto wengi wanapata shida za kumudu gharama za maisha  na masomo kutokana na wazazi wengi kuto kuwa  tabia za kuwawekea  watoto wao akiba ya baadae.

Katika   uzinduzi huo jumla ya watoto  327 walihudhuria   harambee hiyo kutoka shule mbalimbali za wilya ya mpwapwa ambazo ni shule ya msingi Chazugwa,Ilolo, Mazae, Mpwapwa na Kikombo  na kati hao ni watoto  wacache tu walikuwa na akaunti za benki za watoto.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.