WANANCHI WAMKATA MAPANGA MTUMISHI WA HALMASHAURI,KISA KIPINDUPINDU.



Jeshi la polisi wilaya  Mpwapwa Mkoani Dodoma  linawashilikia watu wanne  wa kitongoji cha Isalaza kijiji cha Igoji II  kwa tuhuma za  kumjeruhi mtumishi wa Idara ya afya  halmashauri ya wilaya bwana  Yusuph Ridhiwani ofisa afya akiwa kazini .
Tukio hilo   lilitokea march 03 mwaka huu katika kitongoji cha  Isalaza kijiji cha Igoji ii  wilaya ya Mpwapwa na mkoa Dodoma  baada ya  maofisa afya  wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa kwenda kwenye oparasheni ya kudhibiti kipindupindu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma bwana Giles Mroto amethibisha kutokea kwa kutukio hilo   na amesema chanzo cha  mtumishi huyo kujeruhiwa na siraha za jadi ilikuwa ni  waananchi kuto taka kusumbuliwa katika oparesheni ya kuzuia kipindupindi  ambapo kwa Mpwapwa ugonjwa huo umedumu kwa zaidi ya miezi mitano sasa tangu uingie mwezi nov mwaka jana.
Akiwataja watu wanaoshikiliwa na jeshi alisema ni mwenyekiti  wa Igoji II bwana Gelezi Mlowela,Bahati Mwinyi holo,Eda Cholingo na Elei Udoba.
Kamanda Mroto alisema kuwa watumishi  hao  zaidi  10  walioenda kufanya kazi hiyo kijijini hapo kudhibiti ugonjwa wa kipindu pindu kwa kuwakamata watu wasio na vyoo na kuwatoza faini ndipo wananchi wakajikusanya na kuwashambulia watumishi hao “walikuwa wengi zaidi ya sita wengine  walikimbia  ndipo wakabahatika kumkamata huyo mmoja na kuanza kupiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumkata na vitu vyenye ncha kali”
Kamanda Mroto alisema tayari  watuhumiwa wamefikishwa makahamani na kwa sasa wako maabusu katika gereza la Mpwapwa.
Akisimulia Tukio hilo shuhuda tukio hilo na ofisa afya wa halmasahauri ya Mpwapwa bi Mery Mabagwa alisema  walipofika katika kijiji hicho waligawana miitaa ya kufanya kazi  ndipo walipoanza anza kazi  walipokuwa wakiendelea na kazi walisikia kengele  inagongwa  na ndipo  na ndipo wananchi walipo anza kuwavamia na kuvamia gari ya polisi na kuanza kulipiga mawe ndipo dereva akaondoa gari na kukimbia nalo  kuanza kuwakimbiza nakumkamata mmoja wao na kuanza kupiga na siraha za jadi.
Mabagwa alisema “baada ya kumpiga na kumjeruhi mwezao   kwa siraha za jadi walidhani  wamemua na kumuacha akivuja damu pale chini  wakati huo polisi wote wamekimbia vichakani kujificha” alieleza  ofisa  huyo
Mganga mkuu  wa hospitali ya Benjamini Mkapa  wilaya hapa  Dkt Said Mawji  amekili mtumishi wake kujeruhiwa akiwa kazini  na alisema walimjeruhi sehemu za kichwani,mkanoni  na  kupiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa fimbo na malungu.
Dkt Mawji alisema  kwa sasa mgonjwa huyo amelezwa kwenye wadi ya namba 4  katika hospitali ya  Benjamini Mkapa  kwa matibabu na alisema “hali yake inakwenda inabadilika badilika   hivyo bado haijatengamaa vizuri kutokana na kupata majeraha  kichwani  lakini kwa sasa anaendelea na matibabu  na tunafanya kila linalowezekana  ili kuweza hali yake iweze kutengemaa.”alieleza

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.