WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA DODOMA.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekamata wahamiaji haramu 64 ambao ni raia wa Ethiopia pamoja na madereva wawili waliokamatwa katika eneo la Chenene wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakitokea nchini Kenya kuelekea nchini Afrika kusini .

Watu hao walikamatwa walikuwa kwenye roli lilosheheni mabox ya maji kwa ajili ya kuwaficha wahamiaji hao ambapo wamekutwa wakiwa na kiasi cha  fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 5.
kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema wahamiaji haramu wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za udanganyifu ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahamiaji haramu wanaoingia nchini.

Peter Kundy ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji mkoa wa Dodoma amesema jeshi la uhamiaji mkoa wa Dodoma limejipanga katika kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu linaloonekana kushika mkoa wa Dodoma hapo.

Kutokana na hayo wito unatolewa kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uwepo wa wahamiaji haramu nchini ili kudhibiti kitendo hicho.










Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.