MAENDELEO YA MPWAPWA YAMNYIMA USINGIZI DC,AWATAKA WACHIMBAJI WALIPE KODI.



SERIKALI wilayani Mpwapwa Mkoni Dodoma imewataka wachimbaji wadogo wa madini  Kuweza kulipa kodi ya  serikali ili kuweza kufikia Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati  ifikakapo 2015.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri  alipokuwa akifunga  mafunzo ya siku moja yaliyo andaliwa na shirika la wachimbaji madini Wanawake Tanzania(TAWOMA)
Shekimweri alisema kuwa kuwa Mpwapwa pamoja na kujaliwa  madini ya aina nyingi na yadhamani lakini wilaya hiyo aiendani  na maendeleo yalikuwanayo  kitu alichosema kuwa kinatokana  na matumizi mabaya ya rasilimali hizo au usimazi mbovu wa rasilimali hizo  au matumizi mabaya mali hizo ambayo ni za watanzania wote.
ALISEMA “ukiangalia Mpwapwa haiendanani na hostoria  ya wilaya hiyo kimaendeleo japo kuwa na kuwa na Neema ya wilaya  hiyokujaliwa  vitu vingi sasa nataka mlipe kodi ya serikali ilitufikie uchumi wa viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025,lakini tukilipa kodo kwa tutaboresha miradi ya maendeleo ikiwemo reli ya mwendo kasi yaani standand gage”aliongea  Shekimweri.

Mmoja wa wachimbaji wa madini Wilayani hapa Bi Elizabeth Pagama   alisema tangu uongozi wa awamu ya  Tano iingie madarakani hasa Rais Dkt Pombe Magufuli  amekuwa akiwajali  wachimbaji wadogo  na kutaka  wachimbaji hao wachimbe  kwa Tija  na kufuata sheria  za madini  kuwezesha serikali kupata kodi yake kupitia  madini yanayo chibwa  ndani ya nchi.
Kwa upande wake mwenyekiti  wa chama cha wachimbaji madini Wanawake Tanzania Bi Eunice Negele amesema wachimbaji wadogo  wa Madini  endapo  wataweza kulipa kodi ya shughuli wanazo zifanya  kutaweza kutambulika na kuaminiwa na Serikali.
Bi Negele alisema kwa sasa  wachimbaji wadogo  wamekuwa na mtazamo hasi kwa serikali  kutokana  kuwa ni wakwepaji wa kodi kitu walicho kisema kuwa  mkanganyiko   wa sheria za madini kuwa walipe  wapi kunapelekea  wachimbaji wadogo  kuonekana kama sio walipaji kodi.
“Sisi  tuaambiwa kama hatulipi kodi lakini lazima watendaji wa vijiji na kata wajengewe uwezo na sheria za madini juu ya ulipaji kodi  za vijiji,halmasahauri, na seriakli kuu kitu kinacho tuchanaganya”aliongea  Bi Negele.
Bi Negele alisema  kwa sasa  japo kuwa   nchi ya Tanzania inahesabika kuwa na  aina nyingi  za madini na wachimbaji wengi lakini  lakini idara hiyo imechangia kwa asilimia 3%  tu pato katika bajeti ya serikali .
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoani Dodoma (DOREMA) bwana  Kulwa Mkalimoto  aliomuomba   uongozi wa wilaya kuwapo  ulazima wa mfumo mzuri wa ukasanyaji wa kodi na mapato yatokanayo na  madini kwa sasa kitu alicho kisema kuwa kinaishia  mikononi mwa baadhi ya watendaji amabao sio waaaminifu.
  Bi  Doreen Kissia mchimbaji wa kopa katika kijiji cha kinusi alisema   kero wanazozipata kutoka kwa  uongozi wa serikali kwa sasa   ni kutozwa  kodi ambazo hazipo kisheria na  hutozwa na watu ambao si wahusika halali.

Aidha  Bi Kissia  alisema matatitizo  ya namna hii  kwa mkoa wa Dodoma  hasa wilayani mpwapwa  yanaonekana  kuwa sugu  japo kuwa  wizara ya  nishati na madini  kutoa mafunzo   ya sheria  ya madini  na kanuni zake ambayo  viongozi waandamizi  wa wialaya hii walihudhuria mafunzo hayo.
 Aliongeza  kuwa taratibu zinavyozidi kuvunjwa  na baadhi ya  watendaji  kwa maslahi yao, wanaweza kusasababisha uvunjifu wa amani sehemu za migodini hasa kwa wachimbaji wadogo.
Bi Dorren aliiomba serikali kuweza kuharakisha  uuandaji wa tume  ya uchunguzi wa kusafirisha madini nje ya nchi  hivyo ili kuweza kuokoa mitaji yao  ambayo tangu serikali iweke katazo la kusafirisha madini nje ya nchi wamekuwa hawafanyi kazi na kusababisha  kula mitaji na baadhi  yao mitaji yao imekata.
 Pia alisema  urasimu  huo unaoendelea kwa wachimbaji wadogo utakwamishwa  kuongeza pato la mtu mmoja mmoja  na malengo ya taifa ya  Tanzania kufikia  kipato cha kati   ifikapo  mwaka 2025.
 Na aliongeza kuwa  japo kuwa   Dodoma kuwa na aina nyingi  za madini   yanaweza kuinua  hali ya maisha  ya wananchi   na kuchangia  kwa kiasi  kikubwa pato la taifa  lakini halmashauri  ndio zinazorudisha  nyuma  juhudi  hizo kutokana na urasimu uliopo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.