WALEGWA WA TASAF MPWAPWA WATAKIWA KUBADILIKA.

Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Tasaf wilayani Mpwapwa bi Jaribu  Mtwange  akiwa kwe nyumba yake kabla hajajenga  nyumba.
Ofisa ufuatiliaji wa TASAF wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Hosea Sichone  amewataka wawanufaika wa mpango wa kunufaika na kaya maskini  Tassaf wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kutimiza masharti ya Mpango huo ikiwemo kusomesha watoto na kuboresha huduma za afya ili kuweza kuwa na mafanikio yaliyo kusudiwa ya mpango huo.
Sichone aliyasema   hayo mjini hapa katika zoezi la uhuwilishaji wa fedha katika malipo ya fedha kwa walegwa kwa kipindi cha  mwezi March –Apri 2018.
 Aidha Sichone amesema  kumekuwa na upotoshaji mkubwa  kutoka kwa jamii kuwa serikali inatoa fedha hizo bure tu kwa walegwa kitu alicho kisema kuwa  madhumuni ya  mpango  huo ni kuziwezesha kaya maskini  sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu  kuziwezesha kaya hizo kuwa na pesa za matumizi wakati  wa hari,
Ameongeza kuwa  pia madhumuni mengine  ni kuwekeza katika rasilimali watu  hasa watoto katika Nyanja ya Elimu na Afya ikiwa na lengo la kuaandaa kizazi chenye tija ,kuimarisha  shughuli za kuongeza kipato na kuongeza shughuli za  huduma za jamii.
Hata hivyo Sichone  alidai kuwa  mpango huo tangu uanze kutekelezwa mwaka 2014 umeweza kusaidia wanufaika wengi kwa kuongeza makazi bora ,kuongeza kipato cha familia  lakini imeongeza ari ya akina mama kutojifungulia katika mikono salama ya manesi na si kwa wakunga wa jadi na majumbani.
 Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Tassaf wilaya ya Mpwapwa Paskal Jeremia  alisema kwa Mpwapwa  ina walegwa  5993 katika vijiji 57 vya wilaya ya Mpwapwa .
Pia alisema kwa wezi marcha –April  wameweza kutoa kiasi cha shilingi milion 370 ambazo ni malipo ya ajira za muda  na malipo ya masharti kwa walegwa. 
Mmmoja wanufaikawa Mpango huo kutoka katika kijiji cha Idilo bi Judith Nohnya alisema kuwa katika maisha yake alikata tama kuwa asingeweza kujenga nyumba ya bati alkini alisema “ baada ya mpango huu kuanza kwa kweli nilikuwa na nyumba duni ambayo niliezekea udongo (tembe) lakini sasa baada ya kuanza kupokea fedha hizi nimenunua mabati 16 na na nimeezeka nyumba yangu bati na sivujiwi tena”alieleza kwa furaha Bi Judith.
  BI Judith ameiomba serikali kuziondoa changamoto  ndogondogo zinazo ukabili mpango huo kama ucheleweshaji wa malipo ya ajira za muda  na kuwapo na mfumo mzuri wa malipo kwa watu wote wenye sifa za mpango huo kulipwa fedha zao na kuwaongeza baadhi ya watu ambao wana shida lakini hawajaingizwa kwenye Mpango.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.