TASAF YAONYESHA MAFANIKIO KWA WALEGWA MPWAPWA



BAADHI  ya WANUFAIKA wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF wilayani Mpwapwa mkoani  Dodoma , ikiwa ni miaka miwili tu tangu mpango  wa uhuwirishaji fedha  kwa kaya maskini  wanufaika yashuhudia njisi ulivyo weza kubalisha maisha yao kutoka hali za chini kwenda hali za unafuu wa maisha.
Mmmoja wa wanufaika wa mapango huo kutoka katika kijiji cha ikuyu kata Luhudwa Bi Anna Mduwile alisema kuwa alisema kabla ya mpango huo haujanza kutekelezwa alikuwa hana makazi ambapo ilikuwa inamlazimu kulala kwenye chumba kimoja na watoto wake wanne pamoja na baba yao .
Aidha Bi Anna alisema  kwamba  baada ya mpango huo kuanzishwa alijitahidi kujenga nyumba ya bati 16  yenye  vyumba viwili na sebure   na kufuga mbuzi ambapo alisema mpaka sasa tangu anze kufuga  amefikisha mbuzi 4  mbao wanasaidia kuinua kipato cha familia yao.
Wakati huo  huo  wanufaika wa mradi huo katika kijiji cha bumira  wamedai kuwa baadhi ya wanufaika wa wa mradi huo  kwa watu wenye umri mkubwa   pesa hizo wamekuwa wakizitumia kununulia maji  ya matumizi ya nyumbani kutokana na uhaba wa maji unao kikabili kijiji hicho.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya jamii ya usimamizi wa mpango huo bwana Lugano  Samsoni  alisema kuwa katika kijiji hicho dumu moja la  maji huunzwa kwa shilingi 700 hadi 1000  ambapo kaya moja inahitji madumu 4hadi 5 kwa siku , kitu alicho kisema  kinashidwa kuwanufaisha wazee walio ktika mpango  huo.
Hata hivyo mwezeshaji  wa mpango huo ngazi ya wilaya bi Hilda Mgomapayo    alidhibitisha mpango huo kuweza kuinuia kiwango cha maisha kwa wanafaika  kwa kuboresha makazi, kubuni biasahara ndogondogo, na kuwasidia watoto wanao soma kuwanunulia mahitaji yao  bila shida.
Bi  Mgomapayo alisema”Kiukweli mpango huu umeweza kuonyesha mafanikio mazuri sana umeongeza idadi ya akina mama wanaojifungulia katika mikono salama , imepunguza utoro wa watoto shuleni kutokana na mlegwa asipo timiza masaharti hayo pesa yake hukatwa hivyo hawakubali pesa ikatwe kwa hiyo wanajitahidi  kuzingatia masharti”alisema Mgomapayo.
Kwa upande wake kaimu mratibu wa TASSAF wilayani hapa Paskal Jeremia alisema kuwa katika kipindi cha mwezi wa julai na Agosti jumla tsh 210,795,454.55/=zimepokelewa kuwezesha zoezi ngazi ya wilaya  na jumla ya wakazi 6256 wamenufaika.
Paskal ametumia fursa hiyo kuwahadhalisha  baadhi ya walegwa wanaopokea pesa na kuzitumia kwa  kinyume cha makusudi ikiwamo kulewea pombe   kitu alichosema  wataweza kuondolewa katika  mpango huo na kuwaingiza wahitaji wengine.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.