DC ATAKA TASISI ZIJIPANGE KUZALISHA KWA TIJA


MKUU wa wilaya ya mpwapwa mkaoni  Dodoma Bwana Jabil Shekimweli namezitaka  tasisi za serikali na tasisi za umma  wilayani hapa  kuweza kutumia  Agizo la kuhamia mjini Dodoma  kama fursa ya kukuza uchumi wa tasisi zao kwa kuongeza uzalishaji zaidi.
Sha kimweli aliyasema hayo alipokuwa akiongea  na wafanayakazi wa  tasisi ya  ya utafiti wa mifugo TARILI Mpwapwa   kwa lengo la kujitambulisha  na kuzifahamu tasisi.
Mkuu wa wilaya huyo alisema  kuwa agizo la  la serikali la kuhamia  Mjini Dodoma lazima litafasiliwe kwa vitendo na tasisi hizo kwa kuzalisha  kibiashara  na kuongeza tija kwa lengo la  tasisi hizo kupata faida .
Aidha alisema  kuwa  serikali ikiwa imeweka mkakati wa kuhami  mjini Dodoma  lazima  tasisi hiyo  ijiwekee mkakati  wa kuzalisha  bidhaa zitokanazo  na  mifugo  kama maziwa,nyama  kwa lengo  la kukuza uchumi wa Tasisi wa Wilaya  pia.
Aliongeza kuwa “unajua ifikapo mwezi desember  mwaka huu  zaidi ya wafanyakazi  wa serikali na tasisi za umma wapatao 100,000 watahamia Dodoma  kutoka Dar –es- salaam  na hivyo wanahama na uchumi wao usio pungua  billion 1.2 hivyo ni kukua kwa uchumi wa mji wa Dodoma ninyi kama tasisi lazima mjipange katika hizo billion 1.2 mtachukua kiasi gani hapo  kwa kujiwekea mkakati mzuri wa uzaishaji”aliongea Shakimweli.
Pia alitaka tasisi  kuweka  muunganiko  na tasisi  zingine  hapa wilayani  ili kuweza kuona  matokeo ya tafiti  zao  kwa wananchi wanao  wanao izunguka tasisi hiyo  katika idara ya kilio na mifugo.
Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa tasisi  Dkt. Eliakunda Nkimbi  alisema  ukosefu wa  fedha unakwamisha  shughuli za kitafiti  kushidwa kufanyika  na hivyo  kushidwa kutoa  matokeo  ya tafiti   kwa jamii.

Dkt. Nkimbi alisema endapo serikali ikiwekeza  katika tafiti za wasomi  changamoto nyingi zinazo ikabili jamii zitapatiwa ufumbuzi wa changamoto zinazo wakabili kama ,umaskini wa kipato, uhaba wa huduma za jamii, na uelewa  mdogo sera mbalimbali zinazotaka kuwapeleka katika unafuu wa maisha.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.