WAKAZI WA KIBAKWE WAPATA CHUMBA CHA UPASUAJI.





 wakazi wa kibakwe
WAKAZI 82,703  wa tarafa ya  Kibakwe  wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  watanufaika na huduma za upasuaji  mala baada ya kukamilika kwa chumba cha upasuaji  katika kituo cha afya cha tarafa hiyo.
Kwa mujibu wa mganga mkuu  wa wilya Dkt ,Said Mawji  amesema kuwa chumba hicho cha upasuaji  ni moja wapo ya miradi ya maendeleo ya afya iliyo anza kutekelezwa  katika  katika mwaka wa fedha  wa 2013/2014.
Mawji alisema mala bada ya kukamilika kwa chumba hicho kitasaidia wagojwa wa tarafa hiyo waliokuwa wakipewa rufaa kwenda kufanyiwa upasujai katika hospitali ya  wilaya na kupunguza usumbufu kwa wagonjwa na kuokoa maisha ya akina mama na watoto.

Aidha Dkt Mawji alisema  jengo hilo japo kuwa lilikamilika muda mrefu lakini halikunza kutumika  kutokana na ushauri wa kitaalamkutoka ka timu ya uendeshaji wa shughuli za afya mkoa RHMT  na timu ya uendeshaji ya wilaya  CHMT kuwa lengo hilo lilikuwa na mapungufu makubwa  kabla ya kuanza kutumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje alidai  jengo hilo limegharimu jumla ya shilingi milion  59,514,299/=ambazo ni michango mfuko wa wa afya (MMAM)pamoja na mchnago wa fedha kutoka bima ya afya iliyo boreshwa CHF.
Maje alisema kwa sasa chumba hicho kimekamilika  na mwanzoni mwa  mwezi septemba  itaanza kutumika na kuwawezesha wakazi wa tarafa ya kibakwe kuweza kupata huduma hizo kirahisi na karibu zaidi.
Hata hivyo Maje alisema  ujenzi wa chumba cha upasujai ni miongoni mwa utekelezaji wa sera ya afya ya kuwa na kituo cha afya kila tarafa na kuwa na chumba cha upasujai .

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.