NDALICHAKO AJIONEA UCHAVU CHUO CHA UALIMU MPWAPWA.




CHUO cha ualimu Mpwapwa kinakabiliwa na uchakavu mkubwa  ambao unatishia afya za watumishi na wanafunzi chuoni hapo
Kufuatia  uchakavu huo waziri wa elimu ya  sayansi , teknolojia  na ufundi  Pr. Joyce Ndalichako  aliutaka uongozi wa  chuo  cha ualimu  Mpwapwa  kuweza  kufanya  tadhimini  ya ukarabati  mkubwa  wa chuo  hicho  kabla hakijanza  kupokea  wanafunzi wa chuo  kikuu cha Dodoma.
Ndalichako aliyasema hayo  mwishoni mwa  wiki  aliotembelea  chuo hicho  kujionea  hali ya chuo hicho  kabla chuo hicho hakiananza kupokea wanafunzi walio kuwa  wakisoma UDOM  kuhamishiwa katika   chuo cha ualimu Mpwapwa kwa lengo  la serikali  kukabiliana  na chanagamoto  ya ualimu wa sayansi  hapa nchini.
Pr,Ndalichako  aliyasemna  hayo mwishoni mwa wiki  alipotembelea   chuoni hapo  kujionea  hali ya chuo hicho ili kukiweka tayari kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa mpango maluum wa walimu ya masomo ya sayansi .
Pr.Ndalichako  alisema pamoja  chuo hicho kuwa cha muda mrefu  lakini kutokana na  na tabia ya uongozi wa chuo hicho kuto kufanya ukarabati wa mala kwa mala na kupelekea serikali kutumia pesa nyingi  kwa matengenezo .
 Aidha Ndalichako alisema baada ya ya chuo hicho kuteuliwa kupokea  walimu wa masomo ya sayansi ambapo chuo hicho kinakadiliwa kupokea wanafunzi 1100 wa masomo ya Sayansi  ambao walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma.
Kwa upande  Mbunge wa wa jimbo la Mpwapwa George Lubeleje  amesema  kuwa  chuo ni  miongoni   mwa  vyuo  vikongwe  hapa nchini  ambacho kilijegwa  mwaka 1892 kikiwa na lengo la  kuwaandaa waafrika  kukuza  Elimu ya kilimo  hapa nchini.
Hata hivyo kaimu mkuu wa chuo cha ualimu Mpwapwa Chacha Marwa alisema kuwa  kutokana  na chuo hicho  kuwa  cha Zamani  hivyo kinakabiliwa  na uchakavu  mkubwa  anaotishia  afya za wanafunzi na wafayakazi wake.
Pia mwalimu chacha alitanabaisha kuwa  kuwa uchavu huo unahitaji zaidi ya shilingi milini 500 li kuweza kukidhi  hadhi ya kuweza  kutoa huduma  bora ya masomo ya sayansi.
Mwalimu Chacha alisema  kuwa kwa sasa chuo hicho  kinakabiliwa na  uchavu wa miundombuinu yake kama viti,meza,vyumba vya madarasa, maabara,  na nyumba za walimu.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.