SERIKALI INAOBWA KUWEKA SHERIA YA KULINDA HAKI ZA MAHOUSE GAIR.


SERIKALI imeobwa  kutunga    sheria  na kuzisimamia  za kulinda  haki  zawatumishi wa ndani  ili kupunguza  vitendo vya unyanyasaji na  ukatili kwa watoto .
Rai hiyo ilitolewa ofisa ustawi  wa  jamii  wa halmasahauri  ya wilaya ya Mpwapwa   Bwana Richard Kiwale  alipokuwa akiongea  na Majira   ofisi kwake kwa mahojiano maluum.
Kiwale alisema  siku za hivi karibuni  kumezuka vitendo vya watoto kuuwawa na  na wadada wasaidizi wa ndani (house gair) kwa kile kinacho hisiwa kuwa ni hali ya kurudisha kisasi kwa njisi wanavyo nyanyaswa na mabosi wao.
Aidha  Kiwale  alisema  kuwa Mabosi wengi wanao waaajili mabinti wa  kuwasidia kazi za ndani wakuwa wakiwanyanyasa na kuwatendea ukatili  mabinti wao wa ndani kitu alicho kisema kuwa kinachangia mabinti hao kurudisha kisasi kwa watoto wanao walea kwa  kuwachinja au kuwachoma moto.
“watoto wengi ndio wamekuwa wakilea watoto wenzao na hivyo   baadhi ya mabos wamekuwa wakiwanyanyasa sana wadada wa kazi kunyanyaswa sana kuwa kunyimwa haki zao kama  mshahara wa mwezi, chakula na kutolewa maneno  makali  ambayo huwafanya watoto hao kukata tama na kuwafanyia ukatili watoto wanao walea”aliongea  Kiwale.
Mmoja wa   wazazi wilaya hapa Bi Skai Thomas  alisema  kuwa ugumu wa maisha kunachangia  sana kuongeza vitendo vya ukatili kwa watoto kutokana  na kuwatumia watu wa kati wa kuwatafutia  mabinti hao huko vijiji bila kujua  historia ya tabia yake .
Kwa upande wake  mkuu wa Dawati la njisia  katika kituo cha Polisi wilayani hapa  Bi Elfrida Mapunda  alikiri kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto hasa mabinti wa kazi za ndani kutokana na kuwa na umri mdogo  na lakini bila kuwapo kwa sheria za kulinda haki zao.

Pia aliongeza kwamba  lazima walezi na wazazi hapa nchini kujikita katika kusimamia haki za mabinti wanao wasaidia kazi za ndani ili kuepuka vitendo mabyo vimeanza  kusika kasi hivi karibuni vya watoto kuuwawa na watoto wa  mabosi wao.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.