UCHUMI WA MADINI UTAKUZA UCHUMI WA VIWANDA NCHINI.




UCHUMI WA MADINI NA  UTASAIDIA UCHUMI WA VIWANDA TANZANIA.

 

 

Tanzania's 'dictator' president threatening national unity: Catholic bishops

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe John Pombe Magufuli.

 

 

Tanzania  ni nchi  iliyojaliwa  na utajiri mkubwa  wa madini  ya aina mbalimbali kama  yenye thamani kubwa kama ,Dhahabu,Fedha,Chuma,zink,Shaba,Nikel,bati Urani na mengine mengi.
Wawekezaji wamekuwa  wakifutiwa na kubembelezwa kujakuwekeza  nchini katika sekta ya madini  ili  nchi iweze kuendelea ,uchumi wa madini ilianza kusikika  kuanzia miaka ya themanini,kufuatia  ongozeko  la ushiriki  wa wawekezaji  wa kigeni  katika sekta hii ya madini.

Tangu mwanzo  ni kwamba madini  yalitumika  kwa kiasi  kikubwa katika  uzalishaji   viwandani hasa kwa  mawe yenye madini.na sehemu muhimu ya biashara ya ndani  na kimataifa,madini yenye  manufaa kiuchumi ambayo  si  metali ni  grafati,baadhi feldisipa,kwatzi,almasi na chembechembe nyingi  ningene zenye  thamani kubwa kutokana na umuhimu wake kimatumizi.
Kutokana  na njinsi  zama za  zinavyo pangwa ,zama za  mawe zama za shaba,nyeusi,bronze,zama za chuma zama za dhahabuna kadhalika.
Mchakato wa  mzima  wa uzalishaji una adhari kubwa kitaifa na kimataifa katika uhusiano wa kijamii kisiasa na kiuchumi.
Ulimwenguni kote ili viwanda viweze kuzalisha hutegemea takribani asilimia 80 ya madini na metali mengi ya madini hayo ambayo hupatikana kwa wingi  Afrika.
Mashirika ya kigeni yalianza kuokodolea macho Tanzania  mnamo nusu  ya pili ya miaka ya themanini,palebaadhi ya mashirika hayo yaliyopopewa leseni za kutafuta na kuchimba madini,kabla ya kupitishwa kwa sheria ya taifa ya uwekezaji (NIPP)ya mwaka 1990 kuanzishwa kwa  kwa kituo  cha kuhamasiosha  uwekezaji ( IPC) .


Sheria hii iliweza kulegeza mashrti  ya sera ya uchimbaji madini ,sheria hii iliondoa kabisa ukiritimba  na udhibiti wa serikali katika msuala ya uchimbaji madini hata pale serikali ilipokuwa na hisa.
Baada ya Rais  awamu ya tano  Rais Dkt John Pombe Magufuli kuingia  madarakani alibaini madudu  katika idara hiyo kuwa pamoja na kuwapo kwa rasimali hii muhimu haikuweza kuisadia Serikali  katika  kutatuaa changamoto za kiuchumi ambapo ilionekana rasimali hiiilikuwa ikiwanufaisha  wawekezaji.
Kufuatia  hali hiyo Rais alilazimika kuunda tume ya kuchunguza   udongo /chembechembe za mchanga ambazo zimeamabatana na aina nyingi za madini  tume iliyo julikana kwa  tume ya makinikia iliongozwa na Pro Mruma .
Baada ya  tume hiyo kuchunguza na ilitoa taarifa yake  tarehe 17.10.2017  iliweza kubaini ,ubadhilifu,uwizi na mikataba isiyo rafiki  kwa serikali inayo pelekea  madini mengi kutoroshwa nje na kuiacha Tanzania ikiambulia  mashimo  na uharibifu mkubwa wa  Mazingira .

Pro Mluma  akisoma taarifa  alisema kumekuwako  utoroshwaji mkubwa  wa madini  uliopelekea hasara ubwa  serikali  na hivyo  kupelekea baadhi ya watendaji wa wizara hiyo kuiuzuru nyadhifa zao  kutokana na kushidwa kusimamia utendaji katika wizara hiyo ambayo ni miongoni mwa wizara  za msingi kiuchumi.
Baadhi ya wananchi wa Mpwapwa  wanampongeza Rais Joseph Pombe Magufuli  na kusema kuwa  tangu aingie madarakani ameweza kusimamia  rasmali za nchi ,utendaji serikali na kupunguza ubadhilifu  wa Fedha  za umma.
Mwenyekiti  wa  waachimbaji  wadogo wa madini mkoani Dodoma  bwana Kulwa Mkalimoto  alisema tangu Rais aingie madaraka  kumekuwako na   mabadiliko makubwa katika idara hiyo  na fursa za wachimbaji wadogo kuanza kuonekana ,kuwezeshwa mitaji,ujuzi ,na mikopo ili kuweza kusogezambele uchumi wa nchi yetu.


Image result for 5 pounds of gold 
Madini ya Zahabu yanavyo onekana.

Bwana Mkalimoto  alidai kuwa  sambamba  na wachimbaji wadogo  kuwezeshwa lakini pia kuna mahusiano yamekuwa makubwa kati  serikali  na wachimbaji hao ambayo hapo awali  haikuwa hiyo ambapo  Mkalimoto anasema yamesabaishwa na utendaji wa Rais wa awamu ya tano katika kusimamia  rasilmali za wanyonge nchini na  hivyo kusababisha  kukua kwa uchumi nchini.

Mmoja  wa watalaamu  na mchambuzi wa masuala ya kiuchumi  na mwalimu wa chuo cha Mipango  mjini Dodoma ambae hakutaka jina lake kutajwa alisema baada ya mwaka mmoja tu Rais   Kuwa madarakani tuliweza kuona ongezeko kubwa la fedha kwenye  miradi ya maendeleo  kama Afya,Maji ,Elimu ,barabara ,na miradi mingine mingi ,lakini pia alisema pia ndani ya mwaka mmoja uchumi wa Tanzania uliweza kukua kwa  kwa asilimia 7 wakati lengo likiwa kukua hadi kufikia asilmia 7.9
Mchambuzi huyo alisema  “Rais amekaliliwa akisema  Nchi hii ni tajiri na ni kweli ni tajiri nchi hii ina  ina aina nyingi za madini  mengine ambayo  hayapatikani  mahala pengine popote duniani lakini  Tanzania yapo na mengine yanazidi kugundulika ni lazima tumsaidie Rais kusimamia utajiri tulio nao katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati  na Tanzania ya viwanda  maana kupanga ni kuchagua”aliongea Mtaalamu huyo.

Mchambuzi huyo alisema ni lazima watanzania watambue Maslahi mapana  ya nchi  na kuacha kulalamika juu ya hali ya maisha bali wajibidishe katika kufanya kazi  na kumsaidia  Rais kufikia Tanzania tunayo itamani ya uchumi wa kati.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.