JAFFO ATOA MIEZI MINNE KWA WATUMISHI IDARA YA MAJI.


Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ametoa miezi minne kwa mamlaka zote za maji nchini kuhakikisha zinafunga dira za maji kwa wateja wake wote kwa asilimia 90 na kuwa na miundombinu ya kutibu maji watakaoshindwa kufikia hapo watachukuliwa hatua.

Waziri jafo ametoa agizo Hilo mjini Dodoma wakati akizindua ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji za makao makuu ya wilaya na miji midogo nchini na kusema hakuna sababu ya watu hao kuendelea kuwepo kama watakuwa wameshindwa kufikia asilimia 90 katika kufunga dira za maji.

Amesema baada ya kipindi hicho cha miezi minne kupita na ikatokea kuna mamlaka ambayo haijafunga dira ya maji atavunja bodi ya mamlaka hiyo na kumfukuza kazi meneja wake kwa kushindwa kutimiza masharti hayo.

Amesema hatua hiyo imefikiwa ili kudhibiti wizi wa maji ambao unafanywa na baadhi ya wateja kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa mamlaka za maji ambao siyo waamifu na hivyo kusababisha mamlaka hizo za maji kujiendesha kwa hasara.



Kaimu mkurugenzi  mkuu wa mamlaka ya udhibiri wa maji na nishati  EWURA NZINYANGWA NCHANY mamlaka za maji 56 Kati ya mamlaka 83 za wilaya na miji midogo nchini hazina miundombinu ya kutibu maji kuua vimelea vya wadudu wa magonjwa hali inayochangia kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko mara kwa Mara.



 DK BINILITH MAHENGE ni  mkuu wa mkoa wa Dodoma alipata nafasi ya kuzungumza kama mwenyeji wa mkoa huo amesema mamlaka za maji zikizingatia ufungaji wa dira za maji katika maeneo yao itasaidia kuweza kujiendesha kwani zitaongeza mapato yao.
  Ripoti hiyo ya EWURA imeonyesha kuwa hali ya uzalishaji wa maji safi na salama katika mamlaka hizo ni 34.3 ya mahitaji yanayohitajika katika mamlaka za makao makuu ya wilaya na miji midogo.
Mwisho.

Virus-free. www.avast.com

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.