KIPINDUPINDU CHAUA 8 MPWAPWA .




 JUMLA  ya watu  8 wameafiriki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu na wengine 189 wamegundulika kuumwa  ugonjwa huo katika wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma tangu ugonjwa huo ulipotiwe kuingia wilayani humo nov 2017 .
Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dkt Said Mawji aliyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa katika kikao cha baraza la madiwani mjini Mpwapwakilicho fanyika hivi karibuni.
Mawji alisema  kuwa mgonjwa wa kwanza  aligundulika  octoba    mwaka jana  akitokea kata ya Chipogoro  na wagonjwa wengine waliendelea kujitokeza kutoka katika kata mbalimbali hadi kufikia wagonjwa  189 tangu ugonjwa huo uanze hadi sasa.
Aliongeza kuwa  hadi kufikia feb  mosi mwaka huu kulikuwa na wagonjwa wapya 14 ndio waliolio lazwa  katika kambi maluum  ya kuwashughulikia  wagonjwa  wa kipindupindu .
Aidha alisema  chanzo kikubwa cha ugonjwa huo katika kata hizo ni kutokana na kuwapo kwa tatizo la uhaba wa maji  na hivyo watu hulazimika kutumia maji ambayo si safi na salama  ambayo ni maji ya visima vifupi ambavyo ni visima vya kienyeji ambavyo vimetuamisha maji ya mvua na maji ya mtiririko katika kipindi hiki cha mvua.
“Katika kata zenye ugonjwa wa kipindupindu tatizo kubwa la maji safi na salama  kutokana na  hali ya uhaba wa maji  watu wanatumia  maji amabayo si safi na salama  ambayo ni maji ya visima  vifupi vya kienyeji(mikarama) na maji ya mtiririko ambayo si salama sana”aliongea  aiongea Mawji.
Alisema chanzo kingine   kilicho changia kuenea kwa ugonjwa huo kirahisi ni  watu wengi  katika kata hizo kuto kufuata kanuni za afya  na kuto kuwa na vyoo  hivyo hujisaidia vichakani pia mwingiliano wa watu katika kata za mipakani kama kilosa na Chamwino na Kilolo na,kusababisha  ugonjwa huo kulipuka kutokana na husaidia kusambaza wadudu hao kirahisi na maji machafu kunchanganyika  na maji ya visima.
Alisema  kutokana  hali hiyo wamechukua  hatua y ya kutoa elimu ya kanuni za Afya ikiwamo kuchemsha Maji, yote ya visima  kwa kuyawekea  dawa maluum  ili  kuweza kuua wadudu wote  ambao wanaweza kusambaza  ugonjwa huo kwa watu kirahisi na kuwahamasisha watu kufuata kanuni za afya.
Mawji alisema  kwa  sasa wananchi  wanapatiwa  elimu  ya kuhakikisha  wanaishi  katika  mazingira  salama  ikiwa  ni pamoja  na kuwa  na vyoo  bora  kwa lengo la kujiepusha  na mlipiko wa  magonjwa kama hayo   na magonjwa mengine ya mlipuko.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri alisema  katika kata ambazo wagonjwa wametoka kwa wingi wameuunda kamati za kudhibiti na kutoa elimu  ya kanuni za afya  na suala la usafi wa mazingira ili watu  na jamii hiyo kuishi  katika mazingira mabayo ni salama zaidi ambazo kamati hizo zinaongozwa na madiwani wa kata.
Katika  wilaya hii tayari kata zilizo kuwa na wagonjwa wengi zilikuwa ni Iwondo,Mtera,Rudi,Masa Chipogolo na Mlunduzi
Kwa sasa katika mkoa Dodoma wilaya ya Mpwapwa ni miongoni  mwa wilaya ambayo ugonjwa wa kipindupindu umeumkumba kwa kasi  ukiachilia  mbali   wilaya ya kilosa Kongwa,Kilolo mkoani Iringa .
Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.