MVUA ZASABABISHA MAFURIKO GULWE MPWAPWA



Na Stephen noel –Mpwapwa.
Zaidi ya kaya 30 za kijiji cha Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma hazina mahala pa kuishi kufutia mvua kubwa ilionyesha  usiku wa kuamkia jana na kusababisha nyumba zao kubomoka katika kijiji hicho.
Sambamba na nyumba hizo kubomoka pia mvua hiyo imeharibu hekali 47 zamashamaba ya  mazao mabli mbali yalisomwa na maji .
Diwani wa kata ya gulwe  bwana Gabriel Kizige alisema pamoja na maafa hayo pia yamesabaisha  zaidi ya kaya 50 nyumba zao kuingiliwa  na kusababisha badhii ya mali kuharibika ikiwemo chakula na mali zingine .
Akitotaarifa ya madhara yaliyo patikana  mbele ya kamati ya maafa mwenyekiti wa kijiji cha gulwe Bwana Peter Sogodi alisema kuwa nyumba 30 za wakazi wa gulwe zilimomoka na nyumba 50 zilingia maji na hekali 47 za mazao  mbalimbali ziliharibika kwa kusobwa na maji.
Aidha ofisa mkaguzi wa  njia ya treni Steshen Gulwe bwana Moses Magoha alisema pia mvua hiyo imesababisha hasara katika njia ya reli hiyo  kwa kufukiwa  kwa mchanaga , na  zaidi mita 26  za reli   imeobolewa  na  na mvua hiyo.
Akiongea mmoja wa wananchi  wa kjiji hicho bi Elizabeth Stephen  alisema kuwa  mvua hiyo ilinza kunyesha majira ya saa tisa  alfajili  na kusababisha maafa hayo katika kijiji chao ambapo  pamoja na kuwa kaya nyingi zilikuwa zinakabiliwa na njaa  pia mafuriko hayo yameongezea kwakusoma chakula chote kilicho kuwepo cha kuweza kujikimu.
Hata hivyo bwana  Bakari Mlisho  alisema kuwa  kaya zilizo adhilika na mafuriko hayo  ni zile  ambazo baada ya kuhamishwa na uongozi wa  wilaya ya mpwapwa walirudi tena katika makazi yao ya zamani  ambayo sehemu hiyo ni ya mkondo wa maji na sehemu hatarishi kwa makazi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya ya mpwapwa ambae ni mkuu wa wilaya hiyo  bwana  Mohamed Utaly amewataka waaadhilika wa mafuriko hayo kuto kurudi tena katika makazi hayo  ya zamani ambayo ni hatarishi kwa maisha yao.
Aidha alisema kwa hatua za awali wanachi hao waweze kusaidiana katika uwezo walio kuwa nao,pia serikali itatumia sehemu ya chakula cha njaa kuweza kusaidia kaya zilizo adhirika na mafuriko kwa  sehemu kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.