WANACHI WA MPWAPWA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUWAANZISHIA BARAZA LA ARDHI LA WILAYA.



Na Steph noel Mpwapwa
WANANCHI  wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamemuomba waziri  mwenye dhamana ya Wizara  ya Ardhi Nyumba na makazi  Mhe , Wiliam Lukuvi  kuwaanzishia  Baraza la Ardhi la wilaya kufuati usumbufu wano upata kufuata huduma hizo katika wilaya ya  Dodoma mjini.
Walisema huwalazimu kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 90 hadi 110  kutafuta huduma za kishria juu ya migogoro ya ardhi  na mipaka.
Wanachi hao yaliyasema hayo kwa nyakati tofauti wilayani hapa walipokuwa wakiongea na Majira  juu ya usubufu wanao upata kufutia kutafuta haki zao za migogoro ya ardhi iliyo shindikana ngazi ya mabaraza ya kata  na hivyo huwalazimu kutumia muda mrefu na gharama nyingi, na wengine wakiacha kufuatilia haki zao hizo kutokana na kushidwa  gharama .
Mmoja wa wakazi wa  wilayani hapa bwana Alex Mwarabu  mkazi wa kijiji cha Kisokwe  alisema kumekuwako na usumbufu mkubwa unaotokana na  huduma nyingi za kutafuta haki kuwa mbali na hivyo hupelekea baadhi ya watu kukosa haki zao za msingi hasa za migogoro ya mashamba kutokana mabaraza ya  aridhi ya wilaya kutokuwapo  katika ngazi za chini hasa mawilayani.
Aidha Mwarabu alisema kuwa  kufutia hali hiyo  inachangia kuchochea mogogoro  ya ardhi lakini pia kuongeza uhasama hadi vifo maeneo ya vijijini ambapo ndiko migogoro mingi ya ardhi inazidi kushika kasi hasa katika kipindi hiki.
Aliongeza kuwa “haiwezekani  mtu anaona ana haki yake na inaporwa na wenye nacho na sehemu za kukatia rufaa iko mbali  na hana uwezo ndo maana huamua kuchukua njia mbadala ambayo huweza kusababisha  vifo, au uhasama katika  jamii”alisema Mwarabu
Mwarabu pia aliziomba  mamlaka husika ngazi ya halmsahauri kuweza kuzungukia  na kuona utendaji wa mabaraza ya ardhi ya kata kwa kile alicho kisema  kuwa baadhi ya wajumbe wa mabaraza hayo kuyageuza na kuwa sehemu za kutafutia pesa  kwa kuwanyonga haki zao watu wanyonge wasio kuwa na pesa ndio hunyimwa haki.
Tena alitaka serikali ibadilishe mfumo wa mabaraza  kata ambayo kwa sasa hujiendesha kwa kujitolea kitu alicho kisema kinachochea mianya ya rushwa  na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Mwanasheria  wa halmashauri ya wilaya ya mpwapwa na Wakili  Bi Dorica Doria alikili  halmashauri  kuto kuwa  baraza la Ardhi  la wilaya  , kitu alicho sema kuwa kinaongeza  usumbufu mkubwa  kwa wakazi wa mpwapwa na kata  zake 33.
Hata hivyo Bi Dorica  alisema   kuwa jukumu la kuanzisha  mabaraza hayo yako chini ya Waziri mwenye dhamana  ambae ni waziri wa ardhi nyumba na makazi .
“Sheria ya mabaraza ya Ardhi na nyumba ya mwaka 2002 kifungu cha 22 kifungu cha sheria hiyo namba 167 na 168  ya sheria ya vijiji  namba 14  ya mwaka 1999 inampa waziri mwenye dhamana  kuweza kuanzisha hayo kwa kila wilaya , Kanda  na Mkoa”aliongea Bi Dorica
Lakini alisema kuwa serikali inashidwa kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kuendeshea mabaraza  hayo  ambayo katika kila wilaya hapa nchini.




Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.