WANAWAKE WAOBWA KUTAMBULIWA NA KATIBA

aNa  noel  Stephen  mpwapwa

Mwenye kiti wa umoja wa wanawake  Tanzania( UWT) wilayani Mpwapwa  ZELLY NGOWO amesema kuwa  anaomba katiba ijayo  iweze kumtambua na kumlinda mwanamke  kisheria na kikatiba  juu haki zake za msingi na usawa mbele ya jamii,

 Mwenyekiti huyo aliya sema hayo wilayani mpwapwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  mara baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jumuiya hiyo ulio fanyika  mwishoni mwa  wiki hii   mjini mpwapwa mkoani dodoma

 Bi Ngowo alisema kuwa yeye kama mwenyekiti ana mipango endelevu kwa akinamama na kusimamia haki kwa watoto kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na shule kutokana na kukosa haki zao za msingi za kutopelekwa shule.

Pia alisema wanawake wanaweza kusimamia miradi na kuendeleza miradi ndani ya kikundi kwa kupitia nyaja mbalimbali ili mradi wapatiwe elimu ya kutosha kwenye vikundi watakavyo jiunga kwani wanawake wakiwezeshwa wanaweza.

Bi ngowo alisema kuwa wanawake wengi ni waonga ndio maana wananyenyasika sana  kwa sababu ya kushindwa kusimama wao kama wao  na kufanya kazi kwa  bidii ili waweze  kujikwamua kiuchumi na familia zao

“Kwa sasa kama mimi mwenyekiti nina  mpango endelevu wa kufungua shule ya kujifunza kushona yaani cherehani kwa wakina mama na wasichana ili  wajifunze na kujipatia ajira yao na sio kukaa kutegemea kuletewa”

Alisema kuwa wakina baba wanatakiwa kuwaunga mkono wanawake zao kwa sababu wanawake wakiwezeshwa wanaweza kwanza wanaaminika na jamii kwanini wakina baba wanashindwa kuwaunga mkono wake zao ili waachane na hali ya kutegemea mwanaume  na yeye anaweza kufanya biashara yoyote ile .

Bi ngowo alisema wanawake wote wanatakiwa kuwa kitu kimoja kwani umoja ni nguvu wanatakiwa kupendana na kusaidiana pale inapoonekana pana tatizo kwa mwingine na kuachana na hali ya roho mbaya kwa mfano ukiona mwanamke anagombea nafasi wanawake mnatakiwa kuumunga mkono ili apite kwenye ile nafasi baadae atawasaida  wanawake wenzie ’’

Alisema kuwa kwa sasa kuna nafasi nyingi za kugombea au kuteuliwa wanawake acheni hali ya kuongopa jitokezeni kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali na kuachana na  hali ya kutegemea mume zao kwani maisha ni magumu sana tafuteni maisha na kupeleka watoto shuleni na sio kuwaozesha bado wadogo  waende shule elimu ni mwanga wa jamii kwa mtoto. 
  


  

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.