VYANZO VYA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

NA NOEL STEPHEN  MPWAPWA

Imegundulika kuwa  migogoro mingi ya ardhi hapa nchini inasababishwa na vijiji vingi kukosa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Hali hiyo imegundulika na mwandishi wetu aliyeko wilayani mpwapwa aliyefanya utafiti juu  ya kugundua chanzo cha migogoro mingi inayotokea kati ya wafugaji na wakulima inasababishwa na   vijiji vingi hapa nchini kuto kuwa  na  mipango ya matumizi bora ya ardh.

Akiongea mmoja wa  maafisa ardhi wilayani mpwapwa Edina Nambua  alisema kuwa kwa wilaya ya mpwapwa kuna vijiji  tisa tu ambavyo tayari vimefanyiwa  mpango wa matumizi bora ya ardhi kati ya vijiji  124.

Aidha  Nambua alisema kuwa  sababu nyingine inayao pelekea migogoro kati ya wafugaji na wakulima sehemu za vijijini ni baadhi ya   watendaji wa ngazi za vijiji na kata  kuwa sehemu za kusababisha migogoro hiyo kwa kushidwa kusimamai a sheria no 5 ya ardhi ya mwaka 1999ambayo hupelekea mianya ya rushwa,

Tena  alisema kuwa  mpango huo  unagharama kubwa sana kitu kinachopelekea serikali kushidwa kuvifikia vijiji vyote juu  kutengeneza mpango huo  kwa vijiji vyote  hapa  nchini .

 Alidai kuwa   kati ya vijiji tisa vilivyo fanyiwa mpango wa mtumizi bora ya ardhi  vjiji vitatu vya  Pwaga ,Inzovu na Mingui vimefanywa na serkali kwa kupita  mradi wa  Mpango wa kurasimisha  Rasilimali  na biashara  za wanyonge  Tanzania (MKURABITA).

Na vijiji vingine vilivyo bakia ambavyo ni vijiji vya  Lufusi Galigali Mbuga na kizi  ni vijiji ambavyo vimfanyiwa  mpango huo na shirika la kuhifadhi misitu ya asili TFCG lililoko wilayni mpwapwa katika  kijiji cha mbuga.

Vjiji vingine vilivyo fanyiwa mpango huo ni vjiji vya Chunyu na  Ngh`ambi  ambavyo vimefanyiwa mpango na shirika lisilo la kiserkali la DONET  la mkoani Dodoma .

Naye mratibu wa shirika la AFNET wilayani mpwapwa Bwana  NOEL STEPHEN  alisema kuwa katika hili serikali haina budi kulaumiwa moja kwa moja kwa kupanga  mipango mingi lakini kushidwa kuitekeleza:mfano katika  dira ya taifa ya  ya maendeleo kipengele cha tatu kinacho dai kuimarika kwa uchumi imara na wenye ushindani  kwa kuwa na vianzio   mbalimbali vya uzalishaji  na uchumi ambao unamaendeleo ya viwanda yaliyo karibu   na nchi zenye mapato ya kati” alisema  Stephen

Pia aldai kuwa serikali kama  haikuweza kulifanya hilio mapema wakati tayari kuna viashiria vya watanzania  wengi kuanza kuporwa  ardhi zao na wageni kutoka nchi za jirani  kwa kizingizio cha kuoa au kuolewa   na muungano wa afrika mashariki.

Tena siku za karibuni kulizuka mgogoro wa wakulima na wafugaji katika  kata ya masa amabapo baadhi ya watu  kadhaa walijeruhiwa ambao ni wakulima na mifugo ya wafugaji ilijeruhiwa pia.





Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.