WAMACHINGA WA KIMASAI



Bidhaa za wafanyabiashara wa kimasai




TATIZO la wafanyabiashara ndogo ndogo mjini Dodoma , limekuwa ni mzigo mkubwa kwa wafanyabishara hao kutokana na kushindwa kufanya biashara hizo kwa kusumbuliwa na uongozi wa Manispaa.

 
Wakizungumza na waandishi wa habari ,wafanyabiashara hao ambao wanafanya biashara zao katika eneo la viwanja vya mashujaa mjini hapa wafanyabishara hao walisema kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwao kwani hawajui pa kwenda wao pamoja na familia zao.
 
Mmoja wa wafanyabiashara hao,Musa Mollel alisema kuwa ni vema Serikali iwatafutie eneo maalum ama iwahalalishie eneo wanalofanyia biashara kwa sasa ili walipe ushuru na kuiongezea serikali mapato.
 
Mollel alisema kuwa, hata wao wanaweza kujenga vibanda vyao vya biashara kama watahalalishiwa eneo hilo ili kuepukana na jua na mvua ambavyo ni changamoto katika biashara zao pamoja na adha ya kufukuzwa kila mara na mgambo wa Manispaa.
 
“Hapa tunashindwa kujenga vibanda kwa sababu manispaa wanatukuza,lakini kama wakituhalalishia eneo hili sisi tupo tayari kujenga vibanda na tukafanya biashara zetu kwa uhuru,’’alisema Mollel.
 
Akizungumzia namna biashara inavyofanyika katika biashara katika eneo hilo , alisema wanawategemea wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma lakini akabainisha kuwa pindi wanafunzi wakifunga shule biashara inakuwa mbaya zaidi.
 
Alipotakiwa kuzungumzia kero ya wafanyabisha hao, Afisa habari wa Manispaa ya Dodoma Gisela Mavele alisema kuwa wafanyabishara hao wametengewe eneo la kufanyiwa kazi lakini hawataki kuendea huko.
“Ni kweli tunawasumbua lakini kumbuka tayari tuilishawatengea eneo la sabasaba mahali lilipokuwa tampo lakini hawaendi,hata hivyo eneo hilo halijakamilika bado,’’alisema Mavele.
 
Kitendo cha Manispaa kuwafukuza wafanyabisha ili hali wanafahamau kuwa eneo walilowatengeaq halijakamilika, kinatafrisiliwa kuwa ni uonevu unaosababisha mgogoro kukua zaidi.
Mwisho.

kwa hisani ya Group No 3.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.