WAZIRI ZUNGU AWAPA MATUMANI WANA MPWAPWA.




Waziri  wa mazingira  ofisi ya makamu wa Rais (M) na Mazingira Musa Azzan Zungu akielekea katika korongo la Shaban Robert  kuangalia uharibifu iliosababishwa na  korongo hilo(picha na Mpwapwa habari)
WAZIRI mazingira  ofisi ya  makamu ya Rais Muungano na  na Mazingira Mussa Zungu(MB) amesema wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 imetenga kiasi cha shilingi  billion 17.4 kwa ajili ya kupambana na uharibifu na mabadiliko ya Ikolojia.
Waziri Zungu ameyasema hayo  wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma  alipokuwa kwenye ziara ya kikazi siku  ya moja ya kuona uharibifu wa mazingira  na uharibifu wa Korongo la Shaban Robert linalotishia maisha  ya wakazi wa wilaya hiyo  na miundo mbinu .
Waziri  Zungu  amesema pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi  lakini shughuli za kibinadamu   zimeiweka Mpwapwa  kuwa katika hali mbaya ya Kimazingira.
“ Ofisini kwangu  kuna taarifa ya hili korongo   kuwa linatishia usalama wa maisha na makazi ya watu  pamoja na miundo mbinu ikiwamo madaraja ambayo yamesobwa  lakini pia Mbunge  wenu amekuwa akilipigia kelele sana korongo hili” aliongea Wazir Zungu.
Aidha Waziri Zungu  amesema wizara yake katika kupambana  na uharibifu wa mazingira  na mabadiliko ya kiikolojia  wizara hiyo imetenga kiasi cha shilingi billion  17.4  ambazo zitatekeleza  miradi  5 ya mazingira Tanzania bara na visiwani ambapo alisema mine itakuwa Tanzania bara n mmoja utatekelezwa Nzanzibar kaskazini.
Pia waziri  Zungu ametumia fursa hiyo  kutoa maagizo kwa viongozi wa wilaya ya Mpwapwa  kuendeleza  usimamizi  na utunzaji wa mazingira na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hiyo kuwa miundo mbinu ya madaraja iliyo bomoka  italejeshwa kwa wakati ili kurudisha mawasiliano.


 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  bwana Jabir Shekimweri  akitoa maelezo kwa Waziri wa mazingira.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri     amedai  ofisi yake  kwa kuishirikiana  na ofisi  Baraza la Mazingira(NEMC) Kanda ya kati  wamefanya  tadhimi  ya awali  ya kuweza  kujua ghalama zitakazo weza kutumika  kupunguza athari za korongo hilo kuwa ni zaidi ya billion mbili.

Aidha Shakimwei ameongeza kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira  unaondelea katika milima ya Kibolian  na kwa Mdyanga.

“Mhe waziri uharibifu mkubwa wa mazingira unatokana na watu kuvamia vilele vya milima na kufanya makazi ya kudumu huko lakini baada ya kufunguliwa kwa kikosi cha jeshi huko juu kumesaidia kidigo kurudisha hali ya kawaida” aliongea  Shekimweri.

Pia mkuu wa wilaya amesema  baada ya madaraja kubomoka Ofisi ya Tanroad mkoa wa Dodoma  inajenga daraja la mchepuko ili kuweza kurudisha mawasilino yaliyokuwa wamekatika  katika mji wa Mpwapwa wa magari makubwa.

Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Lubeleje amesema kuwa kwa sasa hali ya korongo lilipofikia ofisi ya Mkurugenzi hailiwezi tena bali serikali kuu iingilie kati kuwanusuru wakazi wa mji Mpwapwa.

Meneja wa TARURA Mpwapwa mwandisi Emanuel Lukumai  amesema ofisi yake tayari imeomba bajeti ndogo kwa ajili kujenga daraja la muda la watembea kwa miguu na wameomba kiasi cha shilingi million 457 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu.





.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.