WATU WAWILI WAFA MAJI GULWE MTU NA MJOMBA YAKE



 MPWAPWA -GULWE AJALI
 Daraja la Gulwe walipokuwa wakioga hao Marehemu
 
WATU wawili Wakazi wa kijiji cha Gulwe wamefariki kufatia  kusobwa na maji   baada ya kudumbukia mtoni walipo kuwa wakioga  katika mto.
Tukio hilo limetokea katika mto kinyasugwi  katika Kata ya Gulwe  wilaya ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma .

Akielezea tukuio hilo Shuhuda wa Tukio hilo na diwani wa Kata ya Gulwe Bwana Gabriel Kazige  aliwataja watu wanaosadikiwa kufa maji kuwa ni Safari Matia(38)  na Maduo Msagati (12) mtu na mjomba  yake  wote wakazi wa Gulwe.

 Wananchi wa kijiji cha Gulwe wakiwa Msibani baada ya kuupata miili ya marehemu.

Aidha Bwana Bwana Kazige amesema  marehemu hao waleenda kuoga mtoni na ndipo  alipodumbuki kwenye maji   na mjomba mtu alipokuwa akitaka kumuokoa  “ wote wawili walizidiwa na maji  na kusobwa  nakufariki.

Mhe Diwani alidai miili yote ya marehemu imepatikana na wanafanya mandalizi ya mazishi .
Pia shuhuda mwingine wa tukio aliyejitambulisha kwa jina la Musa Willson  amesema walikuwa wote mtoni bada ya kuona wenzao wamezama na yeyealienda kuwaokoa alipo ona maji yanamzidi nguvu aliamua kujiokoa mwenyewe.

“Mimi nilikuwa hapa nikawa naangalia nikaona yule dogo alipoteleza maji yakamzidi akashidwa kuogolea  mjomba mtu alivyo ona alitaka kumuokoa lakini naye maji yakamzidi wote wakapelekwa kwenye kina kirefu na kufariki” aliongea  bwana Willson.

Hata  hivyo  viongozi wa kata hiyo wanadai kwa mwaka huu tayari mto huo umeshauwa watu saba  kwa kuzama maji.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.