WALIMU WATOA MSAADA KWA DC WA KUJIKINGA NA CORONA.





MPWAPWA.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akipokea ndoo za maji Tiririka   kutoka kwa katibu wa Umoja wa walimu ambao  ni wanachama wa CCM.

UMOJA wa walimu wilayani Mpwapwa ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekabidhi vifaa vya  kujikinga  na ugonjwa wa COVID 19 unaosabishwa na virusi vya CORONA kwa mkuu wa wilaya hiyo.

Vifaa hivyo vimepokelewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.
Katibu wa umoja huo  Mwl Nelson Nyaombo amesema wameamua kufanya hivyo hili kuweza kuungana mkono na serikali katika jitihada kubwa wananazozifanya za mapambano dhidi ya Covid 19 hapa nchini na  ndani ya wilaya .
Mwl Nyaombo amesema  vifaa walivyotoa ni ndoo 25 za maji tiririka  zenye thamani ya shilingi 300,000/=(laki tatu) ambazo serikali zitatoa muuongozo  njisi gani zitagawiwa .
 


Amesema walimu wananafasi kubwa  ya kuelimisha jamii  kwa njia ya  vitendo   kwa kuweza  kutoa walicho nacho  ili kuweza kusaidia watu ambao hawana  uwezo  wa kununua vifaa vya kujikinga  na Corona.
Afisa  Afya wa wilaya Bi Mery Mabagwa  amesema vifaa hivyo vitasaidia  sana katika mapambano  ya ugonjwa huo  katika maeneo yenye uhitaji  zaidi .
Kwa upande wake  mkuu wa wilaya hiyo Bwana Jabir Shekimweri  amesema  kuwa mchango huo  utakuwa na tija  kwa serikali wilayani Mpwapwa  na kata zake kwa ujumla.
“ Natambua mchango huu katika harakati za kupambana na ugonjwa huu  lakini pia mara nyingi nikizungumza na walimu nawaambia Taifa hili limejegwa na walimu Muasisi wa taifa hili alikuwa mwalimu,Rais wa sasa  pia  ni mwalimu, lazima walimu muwe mstari wa mbele kulipigania taifa hili kama walivyofanya na wanavyofanya  viongozi wa sasa wa taifa hili kwa kuwa wazalendo, kujitambua  na kuitambua jamii mnayoifundisha inataka nini na kuacha kulalamika” aliongea 
Aidha Shekimweri amesema  kwa kufanya hivyo inaonyesha kuwa watumishi wa umma tayari wanaonyesha kumuelewa Rais wa Jamahuri  wa Muungano  katika utendaji wake.
Pia amesema uelewa wa corona kwa jamii  ya Mpwapwa ni mkubwa kwa jamii kutumia maji tiririka  na  vitakasa mikono  na kuvaa barakoa pale amabapo kuna mkusanyiko mkubwa  wa watu kama makanisani ,sokoni  na sehemu za kazi.

 Walimu wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo Jabir Shekimweri.
 
Hata hivyo amesema jamii bado iendelee kuchukua tahadhari  na kuendelea kufanya  kazi  kwa bidii huku tahadhari zikuchukuliwa na alitumia fursa hiyo kuwataka kada zingine za utumishi  kuunga mkono jitihada za  serikali  katika kupambana na ugonjwa wa COVID 19.
Mpaka sasa serikali imetangaza  kuwapo kwa wagonjwa 480 walioambukizwa uginjwa huo na huku 168 kati ya wale wal
io ambukizwa  wameshapona ugonjwa wa Corona.
mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.