WAZIRI WA MAMNBO YA NDANI YA NCHI ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA.


MPWAPWA.


WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Mhe George Simbachawene  amepiga marufuku kwa polisi kukamata wananchi,bodaboda    na kuwanyanyasa  na pia amepiga marufuku  kufanya oparesheni yoyote ndani ya mkoa au wilaya  bila kuwashirikisha wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama.


Simbachawene ametoa kauli hiyo wilayani Mpwapwa alipokuwa kwenye ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Simbachawene amesema kuna baadhi ya polisi wamekuwa wakikiuka  taratibu  na kanuni za kipolisi kwa kuwakamata wananchi na hasa madreva wa pikipiki  maarufu kama bodaboda  kwa kisingizio kama mimi nimewatuma “ kuanzia leo kupitia hapa Mpwapwa natangaza bodaboda wasisumbuliwe na  kukamatwakamatwa pasipo kuwa na sababu za msingi” alizungumza .

Pia amewataka bodaboda wote nchi kuweza  kuzingatia sheria za usalama barabarani  ili kuweza kupunguza ajari na kuweza kuokoa maisha ya wao wenyewe na abiria wao.


Akizungumza na madiwani wa wilaya ya Mpwapwa  amesema madiwani hao waache kulalamika  mbele ya wananchi kwa utekelezaji  wa ilani ya chama cha mapinduzi  waende wakawaonyeshe wananchi kile walichokifanya hata kama ni kidogo.
“ Ninacho waaambiwa  waheshimiwa madiwani tembeeni kifua mbele acheni kulalamika  kwa kileambacho ulishidwa kutekeleza  nenda kaonyeshe kile ulichotekeleza  maana wapo wengine wamebaki kulalamika  tu utafikiri ndo wamechaguliwa jana kama na matatizo hayawezi yakaisha yote  hilo mlifahamu” alisisitiza.
Pamoja na hayo Waziri Simbachawene amabe pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe  amesema  anajifuania utekelezaji wa ilani katika jimbo lake kwa kushirikiana na madiwani pamoja na watumishi wa serikali alisema tayari nimmeaandaa kitabu cha kuonyesha kile nilichokitekeleza  kwa wananchi japo kuwa shida haziwezi kuisha zote kwa wakati mmoja.
Kwa upande wake  mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri  amewataka madiwani hao kujitadhimini ikiwa imebaki miezi michache  kusitishwa kwa udiwani wao katika sula zima la  kuchochea maendeleo  katika kata zao .
Shekimweri alisema yapo maagizo ya kisera ambayo yaliyotolewa lakin baadhi ya kata hazijatekeleza ikiwemo kila kata kuwa na shule ya sekondari alisema katika kata 33 za wilaya ya mpwapwa ni kata 9 ambazo hadi sasa hazina  shule za sekondari za kata , pamoja na zahati kila kijiji    sasa nawaomba jitadhimini ninyi wenywe au mkaaianzishe hiyo miradi.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.