SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI INATISHIA AFYA ZA KINA MAMA.



JAMII imeshauriwa kuziamini  tafiti za kitaalamu  zitolewazo na  Serikali ili kuweza kujiletea maendeleo endelevu au kupunguza athari zinazo weza kujitokeza siku za  mbeleni.
Kauli hiyo imetolewa  wilayani Mpwapwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa na Mratibu wa  masuala ya magonjwa ya Saratani  Dkt,Angel Msaki alipokuwa  akiongea  na Majira fisini Kwake  jana.

Dkt,Msaki alisema serikali ikiwa katika   mkakati  mkubwa wa   utoaji wa kinga  ya  saratani ya mlango wa kizazi  bado kwa wilaya ya Mpwapwa kunaonekana mwamko kuwa duni na kutishia  watu wengi kuto fikiwa  na  na zoezi hilo.

Aidha Dkt. Msaki alidai kuwa   tangu   huduma hizo zianze  kutolewa  hosptalini hapo   kuanzia julai 2017 ni akina mama 530  walifikiwa na huduma  hiyo na kati hayo akina mama  18 walipatikana na  daliiza awali  za mlango wa kizazi na akina mama 10  walifanyiwa matibabu  ya  ugandishaji na akina mama 25  walipewa rufaa kwenda kuchunguzwa katika hospitali kubwa kutokana na kudhaniwa  kuwa na  saratani hiyo.
“ Kwa Mpwapwa  tatizo ni kubwa kiasi kwamba  kwa mafano kati ya watu 530 waliopiwa ni watu  43 waligunduika kuwa na dalili hizo lakini wengine walidahaniwa kuwa  na saratani kabisa ambapo  ni sawa na asilimia  8% hadi 9% ya watu wote walio pimwa.”alieleza Dkt Kihologwe.

Alisema chanzo cha tatizo hilo ni akina  mama  kuanza kujihusisha na  mahusiano ya kimapenzi  wanali na umri mdogo,au kuwa na wapenzi wengi ,au kuwa na mume mwenye wapenzi au wake wengi na watu wanao ishi na virusi vya ukimwi  alisema wako hatarini kupata maambukizo hayo.

Pia alisema tatizo linaonekana ni kubwa kwa wilaya ya Mpwapwa kutokana na Mpwapwa kukabiliwa na  ndoa za utotoni  na hivyo watoto wengi kujiingiza kwenye mahusiano wangali umri  na viongo vyao havijakomaa kwa ajili  mahusiano ya kimapenzi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Jemsi Kihologwe alisema kuwa  saratani ya mlango wa kizazi ni  mabadiliko ya  ya ukuuaji  wa  seli za mlango w kizazi  ambayo husababishwa misuli  au viongo vingine  ndani ya utumbo figo na  sehemu zingine za mwili.

Dkt  Kihologwe  alisema  tatfiti zilizofanywa na shirika la afya Duniani ( WHO )lilibaini kuwa  saratani ya mongo wa kizazi  lina athari kubwa “ ambapo  kila mwaka inakadiliwa akina mama 466,000 wanathibitika kuwa  na  saratani ya mlango wa kizazi  na wengi wao wako katika nchi zinazo endelea”alifafanua Dkt Kihologwe.
Pia alaisema  kwa Nnchi ya Tanzania ni saratani inayo ongoza kwa kusasababisha vifo  vya akina mama wengi ikifuatiwa na saratani  ya matiti ambapo husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote hapa nchini.

Alisema mkakati wa  serikali sasa ni kutoa chanjo kwa  wasisichana  wote wenye miaka 14  ili kuweza kuwakinga  na saratani hii ya mlango wa kizazi na wanakusudia kuwafikia wasichana zaidi 51378.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.