PAROKO KANISA KATOLIKI ATAKA HUDUMA ZA JAMII KUBOREKA MPWAPWA.

Paroko wa kanisa Katoliki Parokia ya Mpwapwa  Pd Daud Ngimba  akihubiri anisani .



PAROKO wa kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Fatima Mpwapwa jimbo  kuu la Dodoma Padre Daud Ngimba imeitaka jamii ya  watu wa Mpwapwa na viongozi wa Serikali  kuweza kutumia fursa ya Serikali kuhamia Mkoani Dodoma  kuboresha huduma za kijamii kama ,  Barabara,shule , Afya na huduma za maji  wilayani hapo.
Padre Ngimba aliyasema  hayo mwishoni mwa wiki   alipo kuwa akitoa mahubiri  kwenye Misa ya  Utatu mtakatifu  na alipokuwa akiutambulisha mkakati wa kanisa hilo katika kujikita katika utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii ya Mpwapwa.
Padre  Ngimba alisema wakristu ,Tasisi za dini   pamoja na serikali za mitaa katika mkoa wa Dodoma  zitaweza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhamisha makao makuu ya serikali kuja Dodoma na kuipandisha hadhi mkoa wa Dodoma kuwa  kuwa jiji kwa kuboresha huduma za jamii na kuyapatia  majawabu maswali ya changamoto   zilizopo katika mkoa huo kwa wananchi wanao waongoza kwa vitendo.
Aidha Padre Ngimba alisema kuwa wilaya nyingi za Jiji la Dodoma ninakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za utenadaji wa mazoea,migogoro na usimamizi duni  wa shughuli za serikali ikiwamo mazingira “kwa sasa ni miongoni mwa mikoa  inayokabiliwa  na chanagamoto za kielimu kwa kuwa na ufaulu duni,  ubovu wa miundo mbinu uchahache wa  hospitali za binafsi ,pamoja changamoto za  huduma za maji vijijini ”aliongea .
Pia alisema viongozi wa kuchaguliwa kwa kushirikiana na  watendaji  wa Halmashauri kuweza kuboresha ujenzi wa  barabara kwa  kiwango cha rami barabara ya Mbabe –Mpwapwa wenye urefu wa kilometa 60 ili kuweza kuchochea  maendeleo ya Mpwapwa kwa  kuwekeza katika sekta ya usafiri pamoja na viwanda.
Pdre Ngimba alisema  watu  binafsi ,tasisi za dini  lazima  ziwe sehemu za utatuzi wa  changamoto  zinazo ikabili jamii ya watu wa Mpwapwa kwa  kuwekeza  katika shughuli za maendeleo.
Hata hivyo alisema “ Mpwapwa ni miungoni mwa wilaya inayo kabiliwa na changamoto nyingi  kama kanisa lazima tuwe sehemu ya utatuzi wa changamoto hizo  kwa kuwekeza katika  sekta ya elimu afya na huduma jamii”aliongea Padre Ngimba.
Alisema katika mkakati wa kanisa ndani ya  miaka mitano wataweza kujenga shule ,Zahati na kuchimba kisima cha maji  amabacho kitaweza kupunguza adha ya wananchi kutafuta maji mbali  hasa kipindi cha kiangazi.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.