UWIZI PUNDA UTAONGEZA UMASKINI VIJIJINI



.
 Serikali imeobwa kuweka mkakati maluum wa kudhibiti  wimbi la uwizi wa punda ngozi ya  Punda  kutokana na  mnyama huyu kuwa katika hatari kubwa ya kutoweka nchini  na hivyo kusabisha kuongezaka kwa wimbi la umaskini kwa jamii nyingi za vijijini zinazo mtegemea mnyama huyu.

Matukio ya uwizi wa punda  yamekuwa yakiongeeka kila kukicha sehemu mbalimbali za wilaya   ya Mpwapwa na mkoa mzima wa Dodoma.
Katika Tukio  lililotokea katika kijiji Mzase kata ya Berege wilayani hapa punda watano wamekutwa wameibwa na kuchunwa ngozi huku mizoga yao ikiwa ametelekezwa porini.

Mmoja wa wanakijiji  hicho  bwana Naftari Asheri amesema kuwa endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa  za kuweza kuokoa uwizi wa punda kuna uwezekano mkubwa wa wanyama hao kutoweka na  na hivyo kusababisha ongezekao la umaskini sehemu za vijijini kulingana na umuhimu wa mnyama huyo katika maisha ya Mtanzania.

Aidha Bwana Naftari alisema kuwa  lazima serikali iweke mkakati  madhubuti wa kukabiliana na changamoto ya kumuokoa mnyama huyo ambae siku za hivui karibuni  amekuwa akiwindwa zaidi  kuliko mnyama yeyote Yule.


Dkt. Kahema alisema kuwa kutokana  na kuzidi kushamili kwa biashara hii ya ngozi za punda katika jamii kunatishia  wanyama hawa kuzidi kupungua siku hadi siku na kusababisha  kupungua kwa nguvu kazi  ya mfugaji wa punda  kila kukicha.

Aidha Dkt Kahema alisema kutokana na  utafiti uliofanywa na  shirika hilo imebaini kuwa  kila siku punda zaidi ya mia moja  wanauwawa kila siku kwa kuchinjwa  kama kitoweo au kwa ajili ya kuuza ngozi  yake katika  viwanda vya wachina vilivyoko Dodoma na Shinyanga na katika jamii.

Aidha  alisema   kuwa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa ndani ya miaka mitatau mbeleni taifa  litakuwa halina mnyama kazi  kama punda kutokana na  biasahara ya ngozi yake  kushika kasi sana katika bara la asia hasa nchini China.

Hata hivyo Dkt Kahema alisema kuwa  kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na punda wasio zidi laki tano  nchi nzima    lakini uwiano wa uzalishaji na  uchinjaji wa  Punda kwa siku haviendani  na kutishia  mnyama huyo   kutoweka kabisa katika jamii.
                                                                                          
Alidai kuwa  Punda amekuwa akifanya kazi za kila siku za mwananchi wa hali ya chini kijijini hivyo mnyama huyu akipotea basi wimbi la umaskini litaongezeka hapa nchini.

“ Unajua kwa sasa punda mzima uanauzwa kwa shilingi laki mbili  wakati kwa mwaka punda anafanya kazi za zaidi ya milioni tano kwa mkulima kama kulima,kuchota maji, kubeba mizigo na  shughuli zote kila siku kwa mkulima”aliongea Dkt Kahema.



Alisema kutokana na ugumu wa maisha ya mnyama huyu uzalishaji wake kwa mwaka umekuwa wa shida ambapo punda hubeba mimba kwa miezi 12 na na huingia joto mala baada ya miaka mitatu hivyo huzalishaji wake umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na upoteaji wake katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.