UGONJWA WA NGURUWE WAWATIA UMASKINI WAFUGAJI MPWAPWA.




BAADHI yawafugaji  katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameingia hasara   kwa  kupoteza mifugo  yao aina ya nguruwe kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa nguruwe   ujulikano kama African swine fever. 
Wakiongea na Gazeti hili  kwa nyakati tofauti   mmoja wa wafugaji  bi Tabitha Simbeye alisema tangu ugonjwa huo  uzuke wafugaji wengi wamepteza nguruwe wengi na hivyo kuwasababishia hasara  kubwa.
 Tabitha  alisema  katika  mtaa wake zidi ya  zizi lake kulikuwa na nguruwe sita wote walikubwa na ugonjwa baadhi alifanikiwa kuwauza kwa hasara na wengine walikufa na kuwazika.
Alisema nguruwe wengi yameathiliwa na ugonjwa  huo  ambapo alisema Nguruwe hutetemeka na kukosa nguvu . kushidwa kutembea.
Aidha mmoja wa  watafiti  wa mifugo kutoka katika Tasisi ya utafiti wa mifugo  TARILI Mpwapwa ambae jina lake hakutaka liiandikwe alisema kuwa  ugonjwa ambao  hutokea kwa msimu  hiyo  na ni ugonjwa unao sababishwa na virusi hivyo ni ngumu kutibika wala kukinga.
Mtafiti huyo alisema ili kuweza kudhibiti ugonjwa huo ni kupiga karantine  za  shughuli zote za mifugo ikiwemo minada   na shughuli zingine zote ili kuzuia ugonjwa huo kuenea kwa wingi. 
 Kwa  upande wake   Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mpwapwa bwana Mohamed Maje  alikili kuwepo kwa ugonjwa,   kuzuka kwa ugonjwa huo  wilayani  kwake huo uliotekea mkoani morogoro na alisema tayari alishatoa maelekezo kwa maofisa mifugo ngazi ya kata na vijiji ikiwemo kusitisha  shughuli zote  zinazohusiana na uchinjaji,uuzaji na na usafirishaji mazao yote yatokanayo na Nguruwe.
Aidha  Maje alisema  ugonjwa huo unaenezwa na kirus na husababazwa kwa hewa na hivyo  kuna hatari ya wafugaji wakapoteza nguruwe wote  ndani ya wilaya maaeneo ugonjwa uliko iingia. Kwa nature ya ugonjwa huu hana dawa wala kinga  na hivyo ukiingia eneo Fulani hakuna njisi  pia kuna wasiwasi wafugaji wanaweza kupoteza nguruwe wote katika maeneo ugonjwa ulipo ingia.
Hata hivyo Maje  alisema kutokana na ugonjwa huo umeweza kuadhiri uchumi wa mwananchi na halmshauri kwa kodi zilizo kuwa ninalipwa na wafanya biashara wa mabucha ya nguruwe na ushuru wa majichio.
Pia aliwataka Wafugaji  kuweza  kujiunga kwenye vikundi  ili kuweza kuwa na sauti ya pamoja na katika kuzikabili  changamoto  za mifugo ikiwemo kinga kwa wanyama wao na matibabu pindi ugonjwa utokeapo.
Pia maje alitumia fursa hiyo   kuwataka wafugaji kuzika mizoga ya nguruwe wanao kufa au kuteketeza  kwa  moto ili kuogopa ugonjwa huo kuendelea kuenea katika maeneo mengine  ndani mkoa mzima.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.