JESHI LA POLISI LATEKETEZA HEKALI 11 ZA BANGI MPWAPWA.




Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya mpwapwa  mkoani Dodoma imekamata na kuteketeza hekali 11 za bangi katika safu za milima  Galigali kitongoji cha Dibulilo.
Kamati hiyo iliyo ongozwa na mwenyekiti wa kamati  ambae ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabiri Shekimweri juu ya oparesheni ambayo ni mkakati wa kupambana  na  madawa ya kulevya wilayani hapa.
Mkuu wa wialaya  ya ampwapwa bwana Shekimweri alisema kuwa  mkakati  wa kutokomeza madawa ya kulevya  ni endelevu   katiika wilaya yake  na hivyo  lengo kuu ni la kukisaidia kizazi cha wana mpwapwa cha sasa na badae   kwa mstakabali wa taifa  zima.
Aidha  Shekimweri  amewataka  watenadaji wa kata na viiji kuweza kuweka mkakati huo kwa nagazi ya kijiji, kata na tarafa .
Alisema “Nina wataka watendaji wote wa kata na vijiji kuweza kuweka mkakati huu wa kupambana na madawa ya kulevya kwa ngazi ya kata na tarafa na yeyete kwenye kata yake ikabainika kuna ulimaji wa bangi   na bila yeye kutoa taarifa  atahusishwa  katika makosa hayo”aliongea Shekimweri.
Kwa upande wake   Mkuu wa polisi  wilayani hapa  bwana Edwin  Mafuru amesema  waliokamatwa kwenye tukio  hilo ni mzee  Felisian Mwamba na mototo wake mwenye umri wa mika 14 mwanafunzi wa darasa la sita.
Bwana  Mafuru  alisema  kuwa kutokana na  Jiografia ya wilaya ya Mpwapwa kuzungukwa na milima kuna wa tu wengi wanaojihusisha na  ulimaji wa Bangi katika  safu za milima Galigali,Kibriani.Chogola ,Chinyika na  Milima  ya Mang’aliza .
Hata  mrakibu wa polisi huyo  alisema  “ haiwzekani  mtu analima bangi miaka mitatu  mfulilizo na anazidi kuongeza eneo  kila mwaka lakini taarifa hazitolewi  hivyo kunatupa shaka kuwa watu wengi wanahusika katika hili wakiwemo viongozi wa vijiji na kata ninaomba iwe mwisho jeshi la polisi halijalala  tutashughulika na kila atakae  jihusisha katika vita hii” alifafanua bwana Mafuru
Mmmoja wa wana  kijiji  hicho bwana  Jastini  Mnyalwao   alisema kuwa  kutokana na watu kupenda maendeleo ya haraka haraka na njia za mkato hujiingiza katika biashara haramu za ulimaji uzaaji na usambazaji wa bangi , kitu alicho kiseema kuwa kinaathiri taifa na kizazi cha watanzania.
Uchunguzi uliofanya na Gazeti hli umebaini kuwa  baadhi ya viongozi wa vijiji na kata wamegeuza wakulima wa bangi kama kitega uchumi  kwa kupewa kitu kidogo ili wawafuchie siri  zaulimaji wa bangi  katika milima hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.