WANCHUO WAMTUMBUA MKUU WAO




SAKATA la la uwajibishwaji  kwa la viongozi wazembe likiwa linashika kasi katika tasisi mbalimbali za umma na za serikali  sasa limemkuta mkuu wa chuo cha wanannchi  Chisalu bwana Sebastian Aweit kuvuliwa madaraka yake kwa muda  na mwenyekiti wa kamati  ya ulinzi na usalama kwa tuhuma mbalimbali.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni  katika chuo cha wananchi Chisalu kilichopo katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa bala baada ya  kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa bwana Jabili shakimweli  ambae ni mkuu wa wilaya hiyo  kummvua  madaraka ya ukuu wa chuo kwa muda, mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi   Chisalu Bwana  Sebastian Aweit  kwa  kushidwa kuongoza chuo hicho .
Shakimweli amesema amefikia uamuzi huo mala baada ya kuona na kujiridhisha  juu za tuhuma  zilizotolewa  na wanachuo wa chuo hicho hadi kupelekea wanafunzi kugoma kuingia madarasani  na kutishia hali ya usalama wa wafanyakazi wa chuo hicho na mali za chuo .
Bwana Shakimweri amesema mkuu wa chuo hicho alikuwa  analalamikiwa na wanachuo hao kuwa amekuwa akiendesha chuo hicho kibabe bila kusikiliza malalamiko yao na kushidwa kuitisha vikao vya  bodi kwa zaidi ya miaka miwili,na kushidwa kufuata miongozo ya uendeshaji wa vyuo vya maendeleo ya wananchi.
Pia mkuu wa wilaya huyo amesema kwamba wanachuo wa chuo cha  maendeleo ya wanachi  (FDC) lakini kwenye mitahani yao ya mwisho ilikuwa inandaliwa na VETA  kitu alichosema kilizua  mgogoro mkubwa kati ya wanachuo na uongozi wa chuo  hicho.
Aidha  alisema kuwa pia wanachuo wa chuo hicho pamoja na kufanya mitihani ya VETA lakini vyeti vyao wakivipeleka kwenye soko la ajira  walikuwa hawatambuliki kutokana chuo chao kuto kuwa na hadhi ya kufanya mitihani hiyo ya VETA.
Hata  hivyo  amesema kuwa  kuna baadhi ya kozi ambazo zilianzishwa chuoni hapo kama ya kilimo na mifugo haijawi kufundishwa tangu zianzishwe lakini wanachuo ilikuwa inawalazimu kujibia katika mitihani yao ya mwisho.
Amesema hata hivyo suala hilo ameichia bodi ya chuo  hicho ili kuweza kuliwasilisha wizarani kwa hatua zaidi.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.