WANASISA NA WATUMISHI WAASWA KUSHIRKIANA KUILETEA JAMII MAENDELEO ENDELEVU.



Na  noel Stephen  mpwapwa.
WATENDAJI  na wanasiasa wilayani mpwapwa wanatakiwa  kushirikiana katika kuiletea wilaya hiyo maendeleo endelevu.
LAI hiyo imetolewa na katibu Tawala wa wilaya hiyo  Athanasia Kabuyanja  alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari ofisi kwake mapema wiki   kwa  mahojianao maluumu.
Kabuyanja  aliwataka  watumishi  na watendaji wa serikali kuweza  kushirikiana  katika kuiletea wilaya hiyo  maendeleo endelevu juu   juu kilimo, utunzaji mazingira, utawala bora na huduma za jamii ili mtanzania aifurahie nchi yake na anufaike na kodi anazo lipa.
ALISEMA kwa wilaya ya mpwapwa ni miongoni mwa wilaya amabazo ziliweza   kuingia  katika migogoro ya kiutendaji kati wa watumishi na wanasiasa  kwa mwaka 2013 kitu alicho kisema kuwa  kwa sasa hali hiyo imetulia    na ushirikiano umemalika.
Aidha  alisema  “kunapokuwa na migogoro   katika halmashauri yoyote ile kuna kuwa hakuna ufanisi wa kazi hivyo watu  wanabaki kutatatua migogoro tu kuliko kufanya kazi za maendeleo za kuwaletea wanachi  maendeleo”aliongea na kuongeza kabuyanja.
Pia   aliwataka watendaji  wote wa kata na vijiji kuzingatia  utawala bora  na misingi yake  ili kuweza kuondoa  kasumba ya   baadhi ya watendaji wa kata na vijiji kuwa ni miongoni mwa viongozi wanao kiuka  misingi ya utawala bora  kwa kuendeleza hongo na rushwa.
ALIWATAKA   wanachi wa wilaya ya mpwapwa kuweza kutoa  taarifa  za ukiukwaji wa  misingi  ya utawala bora  pale ambapo wanapoobwa rushwa  au hongo yoyote  ili kuweza kupata  haki ya kuhudumiwa kitu alicho kisema kuwa kupata haki ni  haki ya kila mtanzania  pasipo kujali kipato, njisi , kabila  wala ukoo wote wanahaki sawa  mbele ya jamii na sheria.


Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.