UHABA WA MAJI MPWAPWA



 Na noel Stephen –mpwapwa
Kuna uwezekano mkubwa  wa kuzuka kwa magonjwa milipuka  kama kipundupindu na magonjwa ya  kuambukizwa katika  tasisi nyingi  zikiwemo vyuo, shule za sekondari  na maeneo ya mikusanyiko ya watu wilayani mpwapwa mkoani Dodoma kutokana na kukosa  huduma yamaji kwa siku tatu mfululizo sasa.
AKIONGEA  na mwandishi wetu wilayani hapo  kaimu mkuu wa shule ya sekondari  ya mpwapwa Sisti Karia  alisema kuwa katika shule yake kumekuwako na hali mbaya  kiafya hasa maeneo ya vyooni  kutokana na kukkosekana kwa maji  katika shule hiyo.
 Alisema kwa sasa shule hiyo imeamua kuendesha shule  kwa maji ya kununua katika matoroli   ambapo kwa dumu wananunua  sh 500/=hadi  1500/=kwa dumu la lita ishirini ambapo alisema napo hali hiyo haitoshelezi  mahitaji  ya shule kwa wanafunzi kuoshea vyombo,kuoga na kuendea vyooni”kwa sasa tuna hali mbaya sana hasa vyooni  maana maji haya yanatosheleza kupikia chakula tu hata maji ya kunywa yanakosekana  sasa hali ikiendelea hivyo si tutauwa watoto wa watu hapa endapo magojwa ya mlipuko  yakitokea au homa ya matumbo  tutafanyaje?aliongea Karia na  kuongeza.
AIDHA  mwandishi wetu alipo zungukia katika tasisi nyingi wilayani hapo alibaini hali bado  mbaya hasa katika  chuo cha ualimu Mpwapwa, chuo cha mifugo Visele na sehemu za migahawani.
Kufutia hali hiyo   wilaya hiyo kwa    imekosa huduma ya nyama kutokana na wachinjaji kuto kuchinja kwa sababu ya kukosa maji ya kuoshea nyama hizo   ambapo watu wengi hasa wafanya biashara ya nyama wameingia hasara kutokana na hali hiyo.
Kwa upande wake meneja wa   mamalaka ya maji safi na maji taka  MPWAUSA SHADRECK  MATEMBA amesema tatizo hilo limetokana  na kuungua kwa Transifoma  ya umeme karibu na kisima  chao cha maji kilichopo  vianze kikombo.
Pia ameongeza kuwa  kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha wilayani hapo  miundo mbinu  mingi ya maji imeng’olewa na mvua hivyo kusababisha maji kuto ingia katika matenki yake,
Na alisema kutoka na kuanguka kwa nguzo tisa  za umeme eneo la chalinze  nalo limechangia  maji kuto kurudi kwa muda ulio kusudiwa  wilayani hapo.
Matemba amewataka wanachi kuwa wavumilivu    wakati mamlaka ya maji  wilayani mpwapwa wakishirikiana na shirika la umeme TANESCO wakijaribu kulitatua tatizo hilo  na kurudisha  katika hali yake ya kawaida.
Wadau wa  maji mjini hapa wameishauri mamlaka hiyo kuto kuwa na chanzo kimoja cha maji  bali wajaraibu kuwa  na vyanzo vingi iwezekanavyo ili kuweza  kuokoa maisha ya watanzania  kwa kuwa na mtanteki makubwa ya kuvuna maji mvua   ili kuweza kuyatumia pindi  inapo tokea dharura kama hii ya kukatika kwa maji siku tatu mfululizo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.