WANANCHI IGOVU WAHAMASISHANA KUFANYA MAENDELEO




Na Stephen Noel.

 Wananchi wa Mtaa wa Igovu kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa mtaa baada ya kumaliza shughuli za maendeleo.
WANANCHI wa Mtaa wa Igovu kata ya Mpwapwa mjini  Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma  wameushauri uongozi wa serikali za mitaa ngazi ya halmashauri kuweza kushirikiana na uongozi ngazi ya mitaa kutumia rasimali walizonazo  kuondoa chanagamoto  ndogondogo zinazowakabili wananchi kuliko kutegemea bajeti   ya serikali kuu.

Wananchi hao walitoa ushauri huo  walipokuwa wakiongea na mwandishi wa habari   jana walipokuwa katika shughuli  za maendeleo za mtaa wa Igovu  kwa kuchimba barabara na  kuweka kufusi  ili kuweza kurahisisha upitakaji wa  njia mtaani  hapo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo bwana Elieza Mwaluko alisema kwa sasa seikali  ina miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa “lakini serikali ngazi ya halmashauri na serikali za mitaa ngazi ya mitaa na vijiji wakitumia raslimali walizonazo watapunguza changamoto ambazo ni kero ya maendeleo kwa wananchi”ameeleza.

Bwana Mwaluko amesema kufuatia mvua kubwa zilozonyesha  mwaka jana zilisababisha barabara  nyingi za mitaani kuharibika  na kusababisha adha kwa wananchi wa mtaa huo  ikiwemo wagonjwa na misiba.


Pia amesema  kutokana na kuharibika kwa barabara hizo kulipelekea baadhi ya watu wenye magari kupaki magari yao kwa majirani kitu alichokisema kuwa kilikuwa kinatishia  usalama wa mali hizo.

Aidha Bwana Mwaluko amesema  wananachi hao wamehamasishana wenyewe kwa wenyewe  ili kuweza kuondoa changamoto ya barabara katika mtaa wao ili kuweza kurahisisha mawasiliano  kati ya mtaa na mtaa.

“Kwa sasa mji wa Mpwapwa umekua kwa kasi kubwa kutokana na kufunguliwa kwa kituo cha JKT Hivyo tuna watu wengi wenye magari   lakini barabara zilikuwa hazipitiki na hivyo iliwalazimu watu hao kuomba kupaki magari yao kwa watu au sehemu za paking kitu kilichokuwa kinawaongezea  gharama  lakini pia kufunguka kwa barabara hizi kutasaidia akitokea mgonjwa,mamamjamzito, au msiba kuweza kumsafirisha kwa haraka tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inatulazimu kumbeka mgonjwa kwa kitanda hadi sehemu ambapo barabara ni nzuri” aliongea

Mmoja wa Wananchi wa mtaa huo na barozi wa  wa mtaa wa Igovu Kaskazini  bwana  Sospiter Magawa alisema  majukumu ya serikali ya mitaa ni kuwajengea uwezo  wananchi  kuweza kutambua majukumu madogo madogo  kama ukarabati barabara ,kutoa nguvu kazi  ila wameiomba  halmashauri kuweza kutoa magari  kwa ajili ya kubeba vifusi  na kokoto pindi zikihatika .

Bi Kathelini Msalila  amesema kutokana na kuharibika kwa barabara hizo kulikuwa kunatishia  usalama kwa akina mama waja wazito  na wagonjwa pindi mgonjwa atokepo nykati za usiku .

“lakini wananchi wakijitoa pia halmashauri utuunge mkono kwa  kupatia japo gari tu ili wananchi wajaze  mafuta  lakini kila kitu tukisubiri bajeti za serikali hatutafika na maendeleo yatachelewa sana Mpwapwa lazima tujenge moyo kwa kujitoa kama wanavyo fanya mikoa mingine” ameongea Bi Msalila.

Kwa upande wa ofisi Tarura Wilaya ya Mpwapwa wamesema  pamoja na barabara hizo kuwa chini ya Tarura lakini wananchi wa eneo husika ndio wamiliki wa barabra hizo kwa kuzilinda na kuzifanyia matengezo kama ya kufikia mashimo na makorongo.

Hata hivyo amesema changamoto inayo ikabili ofisi yao ni kukosa Loli na kusomba vifusi ili kuweza kusaidia wananchi wanajitolea katika ukarabati mdogomdogo wa mitalo ya barabara.
Mwishooo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.