MAHAKAMA YA (W) MPWAPWA YAMFUNGA MIAKA 30 KWA KOSA LA KULIMA BANGI






 MPWAPWA -MWANAWOTA.
Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya  ya Mpwapwa mkoa wa  Dodoma  imemuhukumu kifungo cha miaka 30  jela    bwana  Julius Lwagila (52) baada ya kupatikana na kosa  kulima  na kuhifadhi madawa ya kulevya aina ya bangi.

Hukumu hiyo iliyokwishatolewa  mwaka  2019,na aliye kuwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo bwana Paschal Mayumba lakini haikutekelezwa kutokana  na  mtuhumiwa siku ya hukumu  kutotokea mahakamani.

Hata hivyo  mahakama ilitoa adhabu hiyo  bila mtuhumiwa huyo  kuwapo   mahakamani na mahakama kuamauru jeshi la polisi kumtafuta popote alipo ili atumikie adhabu yake. 

Hukumu hiyo iliyotolewa na aliyekuwa  hakimu mkazi   wa Mahakam ya wilaya Mpwapwa  bwana Paschal Mayumba ambae kwa sasa amehamia mahakama ya  wilaya ya Dodoma. 

Siku ya hukumu  hakimu Mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo    mkazi wa kijiji cha Isasamambo kata ya Mwanawota na wilaya ya Mpwapwa  alikamatwa na jeshi la polisi Mpwapwa likiwa katika oparesheni dhidi ya madawa ya kulevya  ambapo mtuhumiwa alikamatwa akilima shamba la bangi lenye ukubwa wa heka  tatu  na nusu.


Mwendesha mashitaka wa polisi Bwana Willson Mwita  aliiambia mahakama kuwa “baada ya mtuhumiwa kutoroka kifungo jeshi la polisi liliendelea kumtafuta na kufanikiwa kumkamata na kumfikisha mahakamani ili atumikie  kifungo chake”.aliongea

Alisema katika shitaka la awali   kesi hiyo namba  58 ya mwaka  2018 ilimuhusisha mtuhumiwa Julius Lwagila (52)kwa kosa la kulima na kuhifadhi madawa ya kulevya  kinyume na kifungu namba 11(1)(a) na(2) cha sheria ya kuzuia  madawa ya kulevya  namba 5 ya mwaka 2015.

Hakimu  Mfawidhi wa mahakama ya wilaya Bi Nurupuldesia Nassary  alimtaka mtuhumiwa aiambie mahakama kwanini hakutokea mahakani siku ya hukumu.
.
Akipewa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa   aliiambia mahakama kuwa “ Mimi sikutoroka  ila kuna watu walinidanganya kuwa kesi yangu imemalizika na wala nilikuwapo nyumbani tu sikuenda popote nashangaa kuja kunikamata ” alijieleza.

Hakimu Nassary alisema maelezo yake hayana mashiko hivyo  anatakiwa kutumikia kifungo kilichotolewa na mahakama  hapo awali.

Mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama kumpatia hati ya nakala ya hukumu ili imsadie kukata rufaa.



.Bwana Julius Lwagila akisindikizwa na polisi kwenye Mahabusu ya Mahakama akisuburi kwenda Gerezani baada ya kifungo chake  kuthibitishwa na hakimu Mfawidhi.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.