UHARIBIFU WA MAZINGIRA WATISHIA JAGWA.









 Baadhi ya akina mama wakipanda mti katika kata ya Mazae

KUFUTIA uharibifu mkubwa wa mazingira  unaofanywa na watu katika  wilaya ya  Mpwapwa  kunatishia  kupungua kwa  upatikanaji wa  huduma ya maji  kwa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Mpwapwa.
Hali hiyo imetanabaishwa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri kwenye  kilele cha siku ya  mazingira  duniani iliyofanyika katika kijiji cha Idilo kata ya Mazae.
Shekimweli amesema  uhai na ustawi wa wa  Taifa letu unategemea  sana  mazingira  yanayotuzungunguka  hivyo alisema uharibifu wa mazingira  ni moja  kati  ya tishio  kubwa la uhai wa binadamu na viumbe vingine  vinavyo tegemea mazibgira  katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Aidha Shekimweri amesema  mabadiliko ya  ya tabia  ya nchi  sasa  yamekuwa ni tishio  la usalama  wa mataifa  kama ilivyo  kwa ugaidi na vita .
Amesema katika nchi za wenzetu  kama visiwa vya  Maldives ambako  mabadiliko ya  ya nchi  yanatishia  kuvifuta  visiwa hivyo  katika ramani  ya Dunia  kutokana  na kuongezeka  na kupanda  kwa kina cha  Bahari” aliongea  Shekimweri
Hata hivyo Shekimweri amewataka  maofisa mazingira wote  wilayani kuweza kueneza  elimu na teknolojia ya  matumizi wa nishati mbadala kuliko kubaki kuitangaza kama nadharia  na elimu hiyo kuwa mjini na kuwaacha watu wa vijijini ambao ndio kundi kubwa linalo husika katika  katika matumizi na uzalishaji wa nishati ya mkaa na kuni.
Diwani wa kata ya Mazae Mhe Wiliam Vahae  aliomba serikali kuweza  kubadilisha  sheria ya  ya kutoza faini au  kuwanyima msamaha watu wote wanapatikana na hatia za uharibifu wa  mazingira kutokana na  na madhara yatokanayo  na uharibifu wa mazngira kwa sasa.
.
Kwa upande wake Ofisa mazingira  wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Teodory Mlokozi  amesema kuwa  kuwamadhumuni  ni kuhamasisha jamii  na duniani kuweza  kuelewa masuala yanayo husu  hatua za kuhifadhi mazingira  na kutoa fursa kwa jamii  kufahamu  kwamba  jamii ina wajibu  wa kuzuia  madhara  na mabadiliko  hasi  katika  mazingira na  kufurahia  yao na vizazi vijavyo.
Pia amesema Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambayo haiku vizuri katika utunzaji wa mazingira  hivyo ametumia fursa hiyo  kuwataka wanajamii kuweza  kutoa taarifa za watu wanao husika katika uharibifu wa mazingira.


Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.