LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.








SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu  waliopatiwa fedha za ukarabati  wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa barabara hizo  sambamba na uboereshaji uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  Jabir Shekimweri alipotembelea  barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea  katika kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa.
Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati  ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na barabara ya kata ya Rufu yenye urefu  wa kilometa  kilometa 16 pia
Shekimweri alisema  hakuna zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali  ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango cha uchumi katika kata zao  ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati.
“Haiwezekani barabara zinapendeza zinanga’aa lakini bado uchumi unakuwa chini hivyo  viongozi kata na chama mjipange  sasa vizuri kwa miundo mbinu hii barabara  iendane  na viwango vya  kukua kwa uchumi kuboresha huduma za jamii  kama elimu afya  na uchumi.” aliongea.
Shakimweri alisema serikali imetoa zaidi ya billion  na milion miatano  kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizi ikiwa nalengo la kufungua fursa za kata hizi kiuchumi,kielimu na huduma za jamii..
Meneja wa wakala wa barabara vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa Mwandisi Godfrey Nkinga alisema kutokana na kukamilika kwa barabara hizo  kutafungua fursa nyingi katika kata husika ikiwemo kuboreka kwa huduma za jamii, pamoja na kukuza uchumi wa kata husika kwa kuweza kusafirisha mazao yao kirahisi au wanunuzi kufuata bidhaa hadi kijijini.

Mwandisi wa  wa anayesimamia ujenzi wa barabara ya Wota hadi Mwanawota Mwandisi Malisa balingumu MATHIAS Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni JP Traders alisema  ukarabati huo unatarajiwa kukamilika kabla ya july 27 mwaka huu na ukarabati huo unakadiliwa kutumia  jumla ya shilingi milioni 783,000,000/=ambapo alisema mpaka ukarabati umefikia asilimia 40 ya kazi yote.
Naye Mwandishi anayejenga barabara ya Kidege LUFU mwandisi  Malisa  Daniel  wa Kampuni ya Classic Buld(LGS) LTD alisema barabara hiyo ilikuwa haijakarabaitiwa  tangu uhuru  na hivyo ilikuwa inawalazimu wananchi wa kata hiyo hiyo kutumia Punda kusafirishia mizigo yao  au kama kuna mgonjwa walikuwa wanambeba kwenye vitanda ili kufikia huduma za barabara.
Alisema ujenzi wa  huo ni  mpango  serikali wa kuunganisha vijiji vyote kuwa una uhakika wa barabara za uhakika zinazopitika msimu mzima.


Kata za LUFU na Mwanawota  wilayani Mpwapwa ni miongoni kata  kongwe hapa  wilayani zinazotegemewa kwa   uzalishaji wa mazao ya Mahindi, Maharagwe, na mbogamboga ambazo zinaweza  kulisha mkoa mzima wa Dodoma na wilaya zake.


Comments

Popular posts from this blog

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.