JAMII YAFICHA TAARIFA ZA UKATILI.


MTANDAO wa polisi wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umesema kasi ya ukatili kwa watoto inasababishwa na jamii kuficha taarifa za vitendo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati lá njisia katika kituo cha polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda katika maadhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa dawati hilo.
Bi Mapunda amesema kuwa vitendo vya ukatili vinavyodhidi kushika kasi vinasababishwa na jamii kuzidi kuvifumbia macho vitendo hivyo au kamalizana kienyeji bila kufuata sheria na bila kuangalia madhara.
Aidha Bi Mapunda ameitaka jamii kwa kusaidiana na jeshi lá polisi kuweza kushirikiana katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake.
Pia amesema katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao huo kumeongezeka kwa taarifa za ukatili ambazo hapo awali zilikuwa zinafichwa kutolewa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi Selina Chimwaga amesema kuwa kuwa kundi kubwa lá watoto hao wenye mtindio wa ubongo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa matibabu kutokana na kuto kuwa na bima za afya.
Bi Chimwaga amesema watoto wengi wamekuwa wakifungiwa ndani, wengine kunyeshwa pombe na dawa za usingiz ili kuogopa kuwaambia kwa baadhi ya wazazi.  
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2009 kimeweza kuwabaini zaidi ya watoto Zaid ya 5000 wenye matatizo ya utindio wa ubongo wakiwa wanafungiwa ndani na kukosa haki yao ya Elimu na hivyo wengi wao wakiwa watu wazima huwa tegemezi.
Mmoja wa walimu anaye fundisha elimu maalun katika shule ya Msingi Chazugwa bwana Hussein Hussein amesema kuwa watoto wenye ulemavu wa wa akili hufichwa ndani kutokana na Imani potofu uliopo kwa jamii juu ya watoto hao.
Bwana Hussein alisema katika shule yake kuna wanafunzi 21 wakiwamo wasichana 8na wavulana 13 japo kuwa wilaya ina watoto wa Namna hiyo wengi katika wilaya ya Mpwapwa.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.