DC PANGANI AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAOMBEA.



.
Mkuu wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga Bi Zainabu Abdalah  amewataka viongozi wa Dini na  watanzania wote  kote nchini kuweza kumuombeombea Raisi ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wote  ili kuweza kuafanikiwa katika vita kubwa ya kiuchumi wanayo pambana nayo.
Sambamba na hili Bi Zainabu  amewataka akina mama wote kuweza kuwasomesha watoto  wa kike  ambao ndio kundi kubwa linalo adhiliwa na  haki ya kunyimwa  fursa za elimu kutokana na chanagamoto lukuki zinazo wakabili watoto wa kike.
Bi Zainabu aliyasema hayo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya hiyo alipokuwa akihudhuria msiba wa mama mzazi wa  mkurugenzi wa halmasahauri ya Pangani   bwana Sabasi  Chambasi  ambae ni mzawa wa Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya huyo bi Zainabu  akiwa ndiye mkuu wa wilaya pekee mwenye umri mdogo katika  wakuu wa wilaya wote  hapa nchini alisema “mimi pia ni mtoto wa kike  hivyo natambua changamoto zinazo wakabili watoto wa kike wengi kushidwa kufikia ndoto zao  kutokana na uhaba wa hudumaza jamii kama afya,Elimu, na maji lakini pia mila na desturi zetu za kumtenga motto wa kike pamoja na huduma   uhaba wa huduma za jamii zinazo mgusa moja kwa moja mwananmke” aliongea.
 Mkuu wa wialya ya Pangani Bi Zainabu Abdalah akiwa katika msiba  Mpwapwa.

Aidha alisema serikali ya awamu ya tano imepania kutetea rasilimali za watanzania  zikiwemo madini,wanayama ,poli pamoja na matumizi sahihi ya fedha za umma ili ziweze kuwa na tija kwa  watanzania wote .
“tunaomba tumuombee  sana Raisi wetu  ili avuke katika vita hii lakini pia ninyi maparoko  tunaomba mtusaidie sana kulifanya taifa hili  kwa kutuombea sana kwa maana tunavita kubwa ambayo inakusa maslahi ya watu waliokuwa wamejilimbikizia mali za watanzania kama zao hivyo hii ni vita ya kiuchumi tuombeeni sana”aliongea pia.
Alisema   endapo  rasimali za watanzania zikatunzwa zitawezesha kuimarika kwa huduma za  afya ,maji,pamoja na elimu ili kuweza kupata taifa  linaloweza kukidhi katika ushandani wa ajira na kuwezesha Tanzania kuingia katika serikali ya viwanda.
Kwa upande wake paroko  wa kanisa katolilki parokia ya Makle alieongoza misa hiyo Padre Gaitano Mwaswenya    aliwataka watanzania kuacha kubaguana kwa ajili ya dini,ukabila   pamoja na vyama vya siasa ambavyo vinaonyesha dalili ya tabia hiyo kuanza  kutamalaki katika taifa lililojengwa  katika misingi ya umoja,
Padre Mwaswenya alisema  kusudi la Mungu kwa binadamu  ni upendo  kati ya binadamu na binadamu mwezie  pia upendo kwa mungu  ili taifa liwe na umoja  na kuondoa tofauti zilizopo kati yetu zinazo sabaishwa na utafauti wa dini,ukabila ,na vyama vya siasa.
Kwa upande wake Mbunge wa  wa Pangani  bwana Juma Aweso  alisema akina mama wakisimama katika malezi  na kutekeleza  wajibu wao watalisaidia taifa la Tanzania  kuimarika kwa  maadili  katika jamii,
Pia Aweso alimtaja  Marehemu  Ritha Sengimba Kama mama shujaa kwa malezi ambae alikuwa na elimu ya kawaida  lakini aliweza kuwasomesha watoto wake ambao wana tija kwa taifa lote la Tanzania  hivyo alitoa wito kwa wazazi wekeza katika elimu kwa watoto wao  ili wawe na tija kwa taifa lote la Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.