Mpango wa PWP TASSAF MPWAPWA UTASAIDIAMAZINGIRA




Imeelezwa   kuwa   shughuli za  ajira muda zilizofanywa na walegwa wa mpango wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu kama kutunza Misitu ya asili,uvunaji wa maji ya mvua, na utunzaji wa udongo,ikitumika inavyopaswa itaweza kuleta mabadiliko  chanya kwa  jamii  na kuweza kujiletea maendeleo endelevu.
Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa Tassaf wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Paskal Jeremia  alipokuwa akiongea  na waandishi wa habari ofisini kwake juu tadhimini  ya utekelezaji wa mpango wa ajira za muda zijulikanozo kama (PWP)kwa wanufaika wa mpango huo wilayani hapa
Jeremia alisema  rasilimali hizo kama ujengaji wa miundo mbinu ya  kuvuna maji ya mvua, wa  utunzaji wa misitu, na  uhifadhi wa  udongo  ngazi ya jamii italeta mabadiliko  kuwa  mazuri  zaidi  na jamii kuweza kujiletea  maendelea endelevu katika maeneo yao yanayoishi .
Aidha  alisema kwa sasa zoezi hilo limetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 70% katika vijiji vyote  ambavyo  mradi huo ulitekelezwa bali alisema kuna baadhi ya changamotozilizojitokeza kama za malipo ambazo makao makuu yanazifanyia kazi na walegwa watalipwa muda si mrefu.
 Alisema  Mpango wa Tassaf  katika awamu zote tatu umeweza kuonyesha mafanikio  mazuri ngazi ya jamii na halmashauri  kwa walegwa walioko kwenye mpango wameweza  kubadilisha maisha yao kwa kujiibulia miradai midogomidogo na kuweza kumubudu maisha yao ya kila siku.
Hata  hivyo alisema  mapango huo tangu uanzishwe  japo kuwa umeongeza ajira lakini pia umeweza  kupunguza  kiwango cha  umaskini ngazi ya jamii na kusaidia kufikia malengo ya   Mkukuta  pamoja na kufikia malengo ya mileniam  ya kukuza kipato cha kaya mojamoja.
Pia alisema katika wilaya ya Mpwapwa ni na jumla ya wakazi 6,048 wananufaika na Mpango wa kaya maskini japo kuwa kuna zoezi la uhakiki wa walegwa hewa unaenelea katika kata zote za mpango.
Kwa upande  wake ofisa  ushauri naufuatiliaji wa Tassaf  wilayani hapa bwana Hosea Sichone alisema  madhumuni ya  mpango  ni kuziwezesha kaya maskini  sana kuongeza matumizi muhimu kwa jia endelevu  na kuziwezesha kaya hizo kuwa na pesa za matumizi wakati  kipindi kigumu zaidi.
Hata hivyo Hosea alisema kuwa  pia madhumuni mengine  ni kuwekeza katika rasilimali watu  hasa watoto ikiwa na lengo la kuaandaa kizazi chenye tija ,kuimarisha  shughuli za kuongeza kipato na kuongeza shughuliza za huduma za jamii.
Mmmoja wawanufaika wa Mpango huo Bi Maligalitha Chinoga alisema kama jamii itaweza kushilikishwa vizuri na kuto kuingliwa na siasa zoezi hili litweza kuleta mafanikio makuu kwa jamii.
Bi Chinoga  aliongeza kuwa  miradi ya kutoa ajira za muda kwa  kaya maskini  japo kuwa unalenga katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali hewa lakini lakini uharibifu mkubwa wa mazingira katika wilaya yetu unatishia uendelevu wa miradi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.