ASKOFU KINYAIA AWAASA WATANZANIA.




Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dodoma Mhasahamu askofu Beatus Kinyaia  amewataka watanzania kuto kukubali kufa kizembe kwa kungangania  mazoea  ya kuto kupanda mazao yanayostahimili ukame katika kipondi hiki cha mabadiliko ya Tabia ya hali ya hewa.

Askofu  alizungumza  hayo jana  jumapili ya januari Mosi 2017wakati  wa misa katika  Kanisa la Bikira  maria  wa Fatima kanisa la hija  katika Parikia ya Mpwapwa .

Kinyaia  amesema haridhishwi na tabia ya baadhi ya watanzania wengi  kuendelea kung’ang’ania  mazoea ya kuto kukabiliana na ushauri wa watalaam na maafisa kilimo kuwataka kupanda mazao yanayoweza kukomaa mapema  na yanayoweza kustahimili ukame  ili kuweza kupata tija ya kilimo chao

Aidha Askofu  Kinyaia  alisema “siku za hivi karibuni  mamlaka ya  ya utabili wa hali ya hewa imetangaza kuwa katika kipindi hiki cha  msimu wa mvua kutakuwa na mvua chini ya wastani hivyo kuwataka wananchi kuweza kupanda mazao yanaweza kuhimili ukame  na kukomaa mapema kama Mtama , Uwele, Alizeti, na Muhogo”alisisitiza Akofu Kinyaia.

Alisema ni lazima Watanzania katika mwaka mpya 2017 hakutakuwa na mbadiliko ya mtu kama mtu mwenyewe hatakubali kubadilika kifkra, na kimtazamo ,na kufanya  kazi kwa bidii  kwa kujiletea maendeleo yake binafsi  na Taifa nzima.

Alisema kumekuwako na lindi la akina dada kufanya biashara za ngono,uuzaji wamadawa ya kulevya , na biashara zote haramu ambazo ni chukizo kwa Mungu na kwa jamii pia ambazo alisema kuwa ni watu wengi kushidwa kujishughulisha kupenda tabia ya ubinafsi bila kujali matokeo ya kazi wanazo zifanyakwa taifa na jamii nzima,

Hata hivyo  alisema  kuwa katika baadhi ya mikoa ya Dodoma  haitaweza kuwa na njaa kila mwaka endapo wakulima wao wakabadilika na  kulima kwa kufuata  maelekezo ya wataalamu  na kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi na mabadiliko yatabia ya  hali ya hewa.

Kwa wake Paroko wa kanisa hilo Daud Ngimba alisema katika ibada  katika Misa hiyo  kutatolewa kipaimara kwa vijana zaidi 278 ambao walipokelewa katika kanisa  na kuwa wafuasi wa  Kristu walio imarika.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.