KAZI KUBWA KUIONGOZA SERIKLI ILIYO JAA RUSHWA.ASKOFU MKUU ANGLIKANA TANZANIA



Na Stephen noel –mpwapwa
ASKOFU MKUU wa kanisa la  Angilikana Tanzania  Dr. Jacob Chimeledya amesema kuwa  kuna gharama kubwa kutunza na kulinda seriklai iliyo jaa vitendo vya rushwa na ufisadi  kuwa vinaweza  kuhatarisha amani ya  Nchi yetu.
Askofu chimeledya  aliyasema hayo  alipokuwa akihubiri katika     ibada  iliyofanyika katika kanisa kuu  la watakatifu wote  Vinghawe  mjini  Mpwapwa.
Amesema kumekuwako na  na vitendo vya  vya  kuhatarisha amani  ambayo husababishwa na viongozi waliopewa  nafasi na wananchi wanyonge kwa   kujimilikisha  mali  za watanzania wanyonge   kusababisha  kuwepo kwa kundi kubwa la walionacho na wasio nacho kitu alichosema kinasababishwa na ubinafsi   kupungua kwa uadilifu  na kutawala kwa rushwa ndani ya taifa letu.
Alisema vitendo vya ufisadi  vinavyo endelea ndani ya  serikali “vinasababishwa na watanzania wanyonge wanakufa  kwa kukosa dawa hospitalini, akina mama wanakufa kwa kukosa vifaa vya kujifungulia,na watoto  mashuleni  hawana vifaa vya kutosha mashuleni huku mtanzania mmoja namiliki  pesa  ambazo  zinaweza kupunguza matatizo hayo”alisema Askofu Chimeledya .
 Aidha alisema  kuwa   “naipongeza  tume ya katiba  chini ya  kiongozi wake jaji  msatafu Lubuva kwa kuweza  kuahirisha zoezi la  upigaji kura hapo april 30 mwaka lingeweza kulisababishia taifa hasara kubwa na  kutumia vibaya  rasilimali  za watanzania”aliongeza na kusisitiza Chimeledya.
Amesema pamoja  na kuahirisha  zoezi la  kupigia kura katiba pendekezwa aliitaka serikali kuweza   kurekemisha  changamoto zote zilizo jitokeza wakati wa uandikishaji wa kwenye daftari la kupigia kura ili kuweza kupunguza watanzania wengi kukosa haki yao ya msingi na kikatiba  kwa kushidwa kufikiwa au upungufu wa vifaa.
Alidai kuwa serikali ingefanya mapema suala la undikishaji wa daftari la wapiga kura  kabla ya Bunge kuvunjwa ili kuweza kuwapa watanzania nafasi  nzuri zaidi ya kujiandaa  uchaguzi mkuu hapo octoba  mwaka huu.
Pia amewataka viongozi wa serikali kujifunza kwa zoezi zima la katiba hii kutokana na kutofanya maandalizi mazuri kumetokea kuahirishwa ahirishwa kwa zoezi hili kitu alichosema kinachoashiria ni mapungufu katika maandalizi.
Hata havyo alisema vitendo mbalimbali vinavyo endelea katika nchi za  wezetu kama Kenya na nchi zingine  kwa watanzania hasa viongozi wote waliopewa madaraka kuweza kuhakikisha  wanaitunza amani ,kwa kuvumiliana, kuonyana ,kusameheana kwa kuwa ndio maagizo ya mwenyezi mungu kwa kila aliye na dini na asiye na dini.
Aliongeza kuwa kumekuwako na kuteleleka kwa amani, kuteleeka kwa mahusiano katika jamii, na kuteteleka kwa  mahusiano kati ya dini na dini   na amesema tunapopita katika kipindi hiki serikali haina budi kujifunza hayo ili kuimarisha umoja na amanai ya nchi  kwa kushirikana na jamii,
Aliitaka jamii kila mmoja aitafute amani na mwenzeke  kwa kuheshimina na kudhaminiana kwa mjibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Alisema nchi yetu  anamisingi  madhubuti  ya amani  serikali isitungize katika mgawanyiko    kwa kuishadadia mahakama ya kadhi ya ikizidi kuinuliwa kwa mlango wa  nyuma inaweza kuvurugika kwa amani katika taifa lisilo kuwa na Dini kama Tanzania
Alisema tanzania haina dini bali watanzania ndio wenye dini  hivyo   mahakama ya kadhi  isiwe suala la kujadiliwa katika mijadala ya serikali    ili kupunguza mgawanyiko na uvunjifu wa amani kwa kadri ya waasisi wa taifa letu laTanzania.
Pia alisema mauwaji ya watu wenye ulemavu  wa ngozi malbino  kwa mujibu wa katiba  ya Tanzania  inampa kila mmoja haki ya kuishi,pia amedai kuwa kunavitendo vingine  nyuma ya pazia ambapo  sasa hata watoto mapacha wanatafutwa  kwa imani za kishirikina  kwa kile alicho kisema kuwa  ni kupngua kwa hofu ya mungu ya  ndani ya watanzania .

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.