WAFANYA BIASHARA WAILALAMIKIA HALMASHAURI.



Na  Stephen noel mpwapwa
UMOJA wa wafanya biashara wa mazao  na wakulima CHAWAMA wilayani mpwapwa mkoani  Dodoma wamelalamikia  uongozi wa halmasshauri  ya wilaya ya mpwapwa kwa upandisha  ushuru wa mazao bila kuwashirikisha wafanya  wanaya biashara  hao.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na ras fm  mjini hapa wamesema kuwa halmashauri imewapandishia ushuru kutoka shilingi  1000 kwa gunia hadi shilingi 5000 kwa gunia kitu walichosema kuwa  halmashauri inazidi kuwadidimiza zaidi.
Akiongea makamu mwenyekiti wa umoja wa wafanya biashara za mazo(CHAWAMA) wilayani hapa Hamis Ally  amesema  wameshitushwa na uongozi wa halmasahauari hiyo kupandisha ushuru wa mazao bila kushirikiana na wadau,  na bila kuboresha huduma  katika soko hilo,zikiwemo huduma za vyoo, maji na umeme ambapo hulazimu kujisaidia vichakani na kwenye majumba ya watu.
Aidha  Stephano Luhanga mfanya biashara wa karanga pia utaraibu wa utozaji wa  ushuru kwa mkulima umekuwa ni wa kinyonyaji  ambapo alisema gunia moja hutozwa zaidi ya mala mbili  mazao yanapotoka shambani, yanaposafirishwa na yanapouzwa pia hutozwa.
 Luhunga amedai kuwa  pamoja  na kubadilisha   bei ya  ushuru huo ambao halmashauri  ilingia  mkataba na Kampuni ya ADOSTA Limited ya mjini Dar-es –salaam  ambayo ilipewa mkataba wa mwaka mmoja lakini kabla hawajamaliza mkataba kampuni hiyo imebadilisha  bei za tozo za ushuru huo bila kuwashirikisha  wadua na  mabaraza la madiwani.
Hata hivyo wafanya biasahara hao walienda mbali na kuadai uongozi wa halmsahauri umekuwa ikitoa kazi kwa wageni na kuwaacha wazawa  kitu alichosema kina pelekea  wilaya hiyo kushidwa kuendelea  kwa miaka 31 sasa tangu ianzishwe.
Pia wamesema kampuni hiyo ya ADOSTA inajiamlia kufanya hivyo kutokana na ina ubia na kigogo mmoja wa halmasahauri hiyo
Jackson Mwazigila amesema  baadhi ya viongozi wa halmasahauri hiyo  wameigeuza halmasahauri kama shamba la bibi kwa kukusanya ushuru na huku huduma za jamii katika wilaya hii ikizidi kudidimia kila kukicha.
Pia wamesema wakazi wa  wilaya hiyo wakiomba kazi ya uzabuni  au uwakala hawapewi hadi watoe rushwa ,kitu walichosema ndicho chanzo kinacho changia halmasahauri hiyo  kutishiakufa na kushidwa kujiendesha kwa mapato yake ndani na hivyo hujiendesha kwa kutegemea fedha kutoka serikali kuu.
Ras fm aliamua kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri kujua kinachoendelea na mkurugenzi  aka jibu kuwa hajui chochote kutokana  na kuto kuwepo ofisini kwa muda wa wiki tatu sasa, na hivyo hawezi kuzungumzia kitu chochote hadi hapo alipo lazimishwa na mwenyekiti wake wa halmashauri hiyo kutolea ufafanuzi wa suala hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya mpwapwa Mwajina lipinga  alidai wameamua kulifanya hilo kwa muujibu wa sheria kuu ya  biashara ya mwaka 1982 iliyo fanyiwa malekebisho mwaka 2002.
Kauli ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ilikinzana na kauli ya mwenyekiti wa halmasahauri ya wilaya  ambao ilimtaka  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo  kusitisha  ushuru huo na kutaka  wafanya biashara  kuendelea kutozwa bei ya  zaani ya shilingi  1000 kwa gunia kwa kile alichosema kuwa hapo wafanya biashara hao  watakapo elimishwa na kufahamishwa zaidi juu ya tuzo hizo.

Comments

Popular posts from this blog

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.